Senegal: Wadau katika sekta ya uchumi wanasubiri kwa hamu uteuzi wa serikali mpyaSenegal: Wadau katika sekta ya uchumi wanasubiri kwa hamu uteuzi wa serikali mpya

Nchini Senegal, mgogoro wa kisiasa katika ngazi za juu serikalini una athari za kifedha. Kufukuzwa kazi kwa Waziri Mkuu Ousmane Sonko na kutokuwepo kwa serikali kunazua hofu ya benki za uwekezaji kuhusu hatari kubwa ya kutolipa deni lake la nje. Hali hii inaweka shinikizo kwa Bassirou Diomaye Faye huku mashauriano yakiendelea, tangu kuteuliwa kwa Ahmadou Ahminou Lo kama Waziri mkuu mpya siku ya Jumatatu, ili kuunda serikali mpya haraka.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Uchambuzi uliofanywa na shirika la ukadiriaji la Bloomfield kutoka Côte d’Ivoire hauna shaka. Katika taarifa iliyochapishwa siku ya Jumanne, ikirejelea “kuzorota kwa hivi karibuni kwa mazingira ya kisiasa” nchini Senegal, taasisi hiyo ya kifedha inataja hatari za “kuzorota kwa utendaji kazi wa taasisi” katika muktadha wa vikwazo vikali vya kifedha, ikimaanisha deni la umma la 132% ya Pato la Taifa.

“Hatari kwa uwezo wa Serikali kukidhi majukumu yake yote ya kifedha kwa wakati zimeongezeka sana,” shirika hilo la kifedha linasema. Kwa maneno mengine, hatari ya kutolipa deni lake imeongezeka kwa Senegal.

Katika muktadha huu, mkuu wa nchi lazima ateue serikali harakaiwezekanavyo na kupata ungwaji mkono kutoka kwa Bunge ili kutoa miongozo iliyo wazi ya kiuchumi na kifedha. “Mkwamo wowote una athari mbaya,” anasema mchambuzi huyu wa masuala ya kifedha. Pia mbaya zaidi ni kuanza tena kwa mpango unaowezekana na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, ambao unawezekana tu ikiwa serikali itakuwepo. Majadiliano ya kiufundi yamepangwa kuanza tena kuanzia Juni 8 hadi 12.

Senegal inakabiliwa na majukumu makubwa ya kifedha yanayoisubiri, yaani utoaji wa faranga za CFA trilioni 1.2 kati ya mwisho wa mwezi Juni na Julai ili kulipa deni lake. Hii ni sawa na mapato ya bajeti ya serikali ya miezi mitatu, kulingana na sheria ya fedha ya mwaka 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *