Mahakama yazuia mpango wa Kenya na Marekani kuhusu EbolaMahakama yazuia mpango wa Kenya na Marekani kuhusu Ebola

Mahakama Kuu nchini Kenya, imeweka zuio la muda kwa nchi hiyo kuwa na kituo cha karatini, kuwapa hifadhi raia wa Marekani watakaokuwa wameambukizwa virusi vya Ebola.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yamewasilisha shauri Mahakamani kupinga mpango huo.

Kituo hicho kilichojengwa na Marekani katika kambi ya kijeshi eneo la Laikipia, kilitarajiwa kuwaweka karantini raia wa Marekani ambao huenda wakawa wametangamana na watu waliaombukizwa virusi vya Bundibugyo ambavyo vimesababisha mlipuko mpya wa Ebola.

Afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutaka kutambuliwa, amesema kituo hicho kitakuwa na vitanda 50 vya kuwatenga raia hao na kitasimamiwa na wafanyakazi wa afya wa Marekani ambao wanatarajiwa kuwasili nchini Kenya.

Baadaye, maeneo mengine matatu ya watu kutengwa yataongezwa, kila eneo likiwa na uwezo wa kuwahifadhi wagonjwa wanne, lengo likiwa kuwatenga Wamarekani ambao wanaamikia kutangamana na wagonjwa wa ebola katika mataifa ya DRC na Uganda.

Aidha afisa huyo amesema kuwa iwapo wagonjwa hao wataonesha dalili au kupatikana wameambukizwa Ebola, basi watatibiwa kwenye kituo hicho hadi pale watakaposafirishwa katika vituo maalum barani Ulaya.

Kulingana na afisa huyo, Marekani imechukua hatua ya kufungua kituo hicho nchini kenya, ili kupisha safari ya wagonjwa hao, huu akikanusha kuwa ni hatua iliochochewa kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *