Hivi ndivyo Chama Cha Mapinduzi CCM kupitia kwa Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama hicho Komredi Kenani Kihongosi kilivyotafsiri kauli mbiu yake ya kazi na utu Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro baada ya Katibu Mwenezi huyo kuahidi kutoa msaada kwa mkazi mmoja wa Siha ambae ni mlemavu wa miguu akiahidi kumnunulia bajaji.
Tukio hilo limetokea muda mfupi tu baada ya Katibu Mwenezi huyo Kenan Kihongosi mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya stendi kata ya Sanya Juu Wilayani huko ambako yuko kwa ajili ya kufanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali, kuangalia na kuimarisha uhai wa Chama Mashinani lakini pia kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Mara baada ya kumwona mlemavu huyo ambae ni baba wa makamu na kumsikiliza changamoto zake ambapo uhitaji wake mkubwa ulikuwa ni apatiwe usafiri aina ya bajaji ili iweze kumsaidia katika masuala ya usafiri na shughuli zingine Kenan Kihongosi kwa moyo wa utu na wa huruma aliahidi kununua usafiri huo leo.
Tukio hilo sio kwamba limerejesha furaha na tumaini la maisha kwa mlemavu huyo tu bali pia limerejesha imani zaidi ya wananchi kwa chama hicho kutokana na kujali zaidi mahitaji ya mtu mmoja mmoja.
Kenan Kihongosi alihitimisha ziara Wilayani humo kwa kishindo kwa kufanya mkutano huo wa hadhara ambapo aliweza kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi wa papo kwa hapo hali ambayo imeendelea kutoa matumaini makubwa kwa wananchi hao.
Leo May 30 Kihongosi anatarajia kufanya ziara katika Wilaya ya Moshi Mjini Mkoani humo ambapo nako atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa Hospitali ya Mawenzi iliyoko katika kata ya Mawenzi Wilayani humo pamoja na mradi wa Stendi mpya ya Ngangamfumuni iliyoko katika kata ya Mfumuni.
(Feed generated with FetchRSS)