
Vita kati ya jeshi la Kongo na waasi wa AFC/M23 wanaoungwa mkono na Rwanda inaendelea kusababisha idadi kubwa ya watu kuhama makazi yao mashariki mwa DRC. Huko Kalemie, zaidi ya watu 50,000 waliotoroka makazi yao wamesajiliwa katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Miongoni mwao ni Wakongo wanaorejea kutoka kambi za wakimbizi nchini Burundi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu maalum huko Kalemie, Denise Maheho
Petro ni mmoja wa wakimbizi wa hivi karibuni wa Kongo kufika katika eneo la Katanika 2. Alikimbilia nchini Burundi baada ya AFC/M23 inayoungwa mkono na Rwanda kuteka jiji la Uvira. Kwa sasa yuko Kalemie kufuatia mchakato wa kuwarudisha wakimbizi kwa hiari uliozinduliwa mwezi Aprili: “Nilipotambuliwa kwa ajili ya kurudi DRC, sikuweza kurudi katika mji wa Luvungi kwa sababu bado unamilikiwa na AFC/M23. Nilichagua kuja Kalemie. Nilipewa hati na nikafika na familia yangu yote.”
Kiwewe
Akionekana amechoka, baba huyu bado ana kiwewe. Anasema alifanyiwa dhulma wakati wa vita na ana wasiwasi kuhusu afya yake: “Nilipata matatizo. Wakati wa vita hivyo, wanaume sita wenye silaha walinitendea vibaya. MSF ilininihudumi kimatibabu. Lakini sijapona kabisa bado. Na sasa tumewasili hapa Katanika 2.”
Katika eneo la Katanika 2, kamati ya eneo hilo ilimhakikishia mkimbizi huyo hivi karibuni kuhusu huduma yake ya matibabu. Daniel Irenge, mjumbe wa kamati ya watu wakimbizi, anaelezea: “Mara tu mtu anapougua, tunampeleka katika kituo cha afya cha Kifungo. Wagonjwa walio hali mbaya hupelekwa katika hospitali kuu. Kisha tunaandaa ripoti ya matibabu na kuituma hospitalini.”
Kwa sasa, eneo la Katanika 2 lina zaidi ya watu 6,500 waliotoroka makazi yao katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.