
Jeshi la Israel limetangaza leo Jumapili, Mei 31, 2026, kwamba operesheni yake ya ardhini dhidi ya kundi la Hezbollah linalounga mkono Iran “inapanuka hadi maeneo mengine” baada ya wanajeshi wake kuvuka Mto Litani kusini mwa Lebanon, takriban kilomita 30 (maili 19) kaskazini mwa mpaka na Israel. Jeshi la Israel liliteka ngome ya Beaufort kusini mwa Lebanon, kulingana na Waziri wa Ulinzi Israel Katz.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kwamba jeshi lilivuka Mto Litani mnamo Mei 29 kusini mwa Lebanon, na hivyo kupanua ukanda wa eneo linalokaliwa na jeshi lake, huku likiendelea na mashambulizi yake ya anga hadi vitongoji vya kusini mwa Beirut. Jeshi la Israelilimeonya kwamba linachukulia eneo lote la Lebanon kusini mwa Mto Zahrani kama “eneo la mapigano.”
Jeshi hilo lilitangaza kwamba wanajeshi wawili wa Lebanon wamejeruhiwa vibaya katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Israel, licha ya makubalinao ya usitishaji mapigano yanayoendelea kati ya Lebanon na Israel. Katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni, Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salam alilaani “kuongezeka kwa mapigano” kusini mwa nchi, huku akibainisha kwamba mazungumzo yanasalia kuwa “njia isiyogharimu sana” kwa Lebanon.