Siku ya Jumamosi, Mei 30, 2026, ilikuwa siku ya mwisho ya kura za mchujo nchini Nigeria. Vyama mbalimbali sasa vimewateua wagombea wao wote kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Lagos, Liza Fabbian

Siku ya Jumatano, Mei 27, kiongozi wa upinzani Atiku Abubakar alishinda uchaguzi wa mchujo katika chama cha ADC (African Democratic Congress) kwa uchaguzi ujao wa urais. Siku ya Jumamosi, Mei 30, Rais wa zamani Goodluck Jonathan aliteuliwa kuwa mgombea wa chama cha PDP (People’s Democratic Party). Peter Obi – ambaye alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa mwaka 2023 – aliidhinishwa rasmi na chama cha chake cha NDC (Nigeria Democratic Congress). Lakini vyama vyote viwili viililaani shinikizo vilivyokabiliana nalo na juhudi za serikali kuwazuia kukutana.

“Raia ndio watakaoamua” 

Jukwaani, Peter Obi anapepeusha bendera ya NDC, chama atakachokiwakilisha katika kinyang’anyiro cha urais nchini Nigeria. Katika hotuba yake, kiongozi huyo wa zamani wa Chama cha Labour alilaani shinikizo la serikali: “Tunataka kuwa serikali ya watu. Kwa watu na kwa ajili ya watu.” Ni watu ambao wataamua. Leo hali ni ngumu. Vyama vya upinzani vinatendewa kama wahalifu; tunanyanyaswa. Serikali yetu itafanya kazi na upinzani. Tutahakikisha inaendelea kuwepo.

“Jonathan amerudi katika ulingo wa siasa!” 

Huko Abuja, polisi waliwazuia viongozi wa PDP kukutana katika ukumbi wa mikutano waliokuwa wameutenga kwa ajili ya mkutano wao. Walilazimika kurudi nyumbani kwa mmoja wa wanachama wao ili kumteua rasmi rais wa zamani Goodluck Jonathan kama mgombea wao pekee: “Leo, mamlaka imetuthibitishia kwamba rais Jonathan anawatisha. Vinginevyo, mnawezaje kuelezea jaribio lao la kutuzuia kukutana? Nendeni mkawaambie Jonathan amerudi!”

Katibu wa kitaifa wa PDP, Ini Ememebong, alisema kwamba sherehe ya umma itafanyika hivi karibuni ili kumpa rasmi bendera ya chama Goodluck Jonathan. Na upande wa chama tawala cha APC, kilimteua Bola Tinubu, kupepeusha tena bendera ya chama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *