Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Amina Said, amesema wanawake wengi nchini wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo, lakini wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa mikopo kutokana na masharti magumu ya dhamana, hususan hitaji la dhamana za nyumba ambazo wengi wao hawazimiliki.

Amina amesema hali hiyo imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya wanawake wengi kiuchumi, hivyo ameomba Serikali kuweka utaratibu wa kutoa mikopo kupitia taasisi za serikali kwa masharti nafuu zaidi ambayo yatawasaidia wanawake kupata mitaji bila vikwazo vikubwa vya dhamana.

Ameongeza kuwa mikopo hiyo itakapowafikia wanawake kwa urahisi itachochea maendeleo ya jamii kwa ujumla, akibainisha kuwa fedha zinazozungushwa na wanawake huingia moja kwa moja kwenye familia na jamii, tofauti na mitiririko mingine ya kiuchumi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *