“Ipo siku itakuwa nisiku njema kwamba sote tutaongea kwa lugha moja”

Amesema hayo Dkt. Aidah Mutenyo, kutoka Chuo Kikuu cha Kabaale nchini Uganda akiwa miongoni mwa washiriki wanaochagiza kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili.

Anaongea hayo kwenye uzinduziwa awamu ya tatu ya safari ya hija ya “Twende zetu Butiama” alikozaaliwa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa muasisi wa Taifa la Tanzania.

Dkt. Mutenyo ameonggeza kuwa “Hiyo siku ikifika sote tutaketi kwenye meza moja tutaongea kile kilicho sahihi kwa lugha hiyohiyo moja ya Kiswahili na tutaelewana”

UN News/John Kibego Kushoto hadi Kulia, AIGP. Simon Peter Okosh, Dkt. Ronext Kisembo Tendo, Mheshimiwa Ababu Namwamba (Balozi wa Kenya nhicni Uganda) na Prof. Aldim Mutembei kutoka Chuo Kikuu cha Dar-resalam wakiwa kwneye sherehe ya uziznduzi wa awamu ya tatu ya ‘Twende Zetu Butyama uliofanyika kwenye ukumbi wa Four Points By Sheraton Hotel jijini Kampala

Kwa upande wake Balozi wa Kenya nchini Uganda Mheshimiwa Ababu Namwamba ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo amesema “Huu sasa unaanza kuwa utamaduni wetu. Utamaduni wetu ya kwamba kila mwaka tunasafiri hadi Butiama. Tunatoa heshima zetu kwake Mwalimu Julius Nyerere.”

Kwake anaona safari hii ni fursa kubwa kuchagiza utangamano wa bara zima la Africa.

“Na tunatumia fursa hii kujikumbusha ile ndoto ya kuiweka Afrika Mashariki na Afrika nzima pamoja na ile ndoto ya kwamba Kiswahili ni mojawapo ya vigezo. Mojawapo ya njia moja kuhakikisha kwamba tuna ambatanisha na tunaunganisha watu wetu.”

Profesa. Pacifique Malonga kutoka Rwanda akafunguka kuhusu Hayati Nyerere “Kwa hivyo jamani Nyerere ni mtu ambaye alikuwa shujaa. Nimesafiri nchi nyingi. Nimefundisha wazungu kule nje hata Marekani hata Oslo. Lakini sijawahi kumwona mtu rahisi mkarimu, mnyenyekevu safi, yaani kwa maneno mengine ni kiongozi ambaye alikuwa Rais shupavu.”

Naye Profesa. Aldin Mutembei, Mgoda wa Kigoda cha Taaluma za Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar-esalam nchini Tanzania, alihudhuria na kusema

“Siku hii ni muhimu lakini si Uganda tu. Ni siku muhimu kwa Afrika Mashariki kwa sababu ya mambo mawili muhimu. Kwanza ni awamu ya tatu ya Twenzetu Butiama ambayo lengo lake ni kuenzi maono na uongozi uliotukuka wa Mwalimu Nyerere. Na uzinduzi huu siyo tu uamuzi wa Mwalimu Nyerere peke yake, lakini unahusu waasisi wa Afrika Mashariki kwa ajili ya maono yao .”

Mkurugenzi wa shirika la Africa Mashariki Fest lililionazisha safari hii ya Hija, Dkt. Ronex Kisembo Tendo, amesema ‘Twende Zetu Butiama’ mwaka huu 2026 itajumuisha matembezi mengi zaidi.

Kazi hii hakuifanya mwenyewe alishirikiana na wenzake kama hayati Mzee Jomo Kenyata wa Kenya pamoja na hayati Daktari Apollo, Milton Obote wa Uganda. Kwa hiyo, tumeona kama vijana kwamba tutaendelea kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Lakini ni muhimu sana pia kuwaenzi wenzake walioamua kumuunga mkono kwa sababu wangeweza kukataa kushirikiana nayeJumuiya isingefanyika. Kwa hiyo tutaanza safari yetu kwa kwenda Kijiji cha Kokoro A, Wilaya ya Kaskazini mwa Uganda. Huko ndiko alikozaliwa na kupumzishwa Hayati Daktari Apollo Milton Obote, rais wa pili wa nchi ya Uganda. Tutakapotoka huko tutakuja Kampala tutajumuika na wananchi katika sherehe za kuadhimisha siku ya Uhuru wa Uganda tarehe tisa mwezi wa kumi hapa uwanja wa Kololo. Tukitoka hapo tukaelekea Butiama nyumbani kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Chini kuna mdahalo wa kupigabdarubini Jumuiya ya Afrika Mashariki, mwendo kasi na ni nini kinasababisha kudorora kwa kasi ya utangamano wa jumuiya. Baada ya hapo tutaelekea jijini Nairobi nchini Kenya ambapo tutaweka maua kwenye kaburi la Hayati Mzee Jomo Kenyatta pale Bunge la Kenya na mwishowe tutaenda kupiga kambi kijiji cha Gatundu wilaya ya Kiambu ambako alizaliwa Mzee Jomo Kenyatta.

UN News/John Kibego Kikundi cha wanamuziki wachanga wanacheza katika hafla ya uziznduzi wa awamu ya tatu ya ‘Twende Zetu Butyama uliofanyika kwenye ukumbi wa Four Points By Sheraton Hotel jijini Kampala.

Balozi Namwamba akatumia fursa hiyo kuwakaribisha washiriki nchini Kenya. ”Tunajitayarisha vilivyo kuitumia fursa hii vyema na tuweze kumkumbuka na kumuenzi Mzee Jomo Kenyatta kama baba wa taifa letu na baba wa Umoja wa Afrika na vilevile kujiunga na wana Afrika Mashariki wenzetu. “

Akiiongea kwa niaba ya Mkaguzi Mkuu wa Polisi nchini Uganda, AIGP Simon Peter, Okosh ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Opereshaeni za Polisi wa Uganda.

amesema.‘Mara hii ya tatu nataka kuandamana na mahujaji. Kazi yetu kama wanausalama ni kuhakikisha kwamba mko salama na tutahakikisha mko salama nchini Uganda. Watakuwa salama kwenda Murchison Falls na hata Akokoro’

Dkt. Patricia Achan Okiria, Naibu Mkaguzi Mkuu wa serikali ya Uganda amesema ni lazima kumuenzi Nyerere kuwakunbusha wadau kutokomeza ufisadi.

“Lazima tujitahidi kutokomeza ufisadi. Katika kazi yangu, ninagundua kwamba ufisadi unatokea kutokana na mmomonyoko wa maadili kama vile uadilifu, uwajibikaji, ukweli, uaminifu na mengine mengi’

 Kwenye uzinduzi huo pia, ilitangazwa Kamisheni mpya ya Kiswahili ya Muungano wa Africa (AU), Katibu Mkuu wake akiwa ni Dkt. Ronex Kisembo Tendo.

“Kwanza, mimi kama Katibu Mkuu pamoja na viongozi wenzangu Mratibu, wetu Profesa Mutembei na makamishna wote, jukumu tulilopewa ni la kipekee. Ni jukumu la kuhakikisha kwamba tunaunda mbinu za kukieneza Kiswahili barani Afrika na ulimwenguni kote.

Dkt. Mutenyo na Profesa. Malongo ni miongoni mwa makamishina 9 wa Kamisheni hiyo ya “ACALAN – AU Kiswahili.”

Je, malengo yake ni yapi? Makao makuu yake yatajengwa wapi na kwa nini? Jiunge nasi tena tarehe saba Julai siku ya kimataifa ya Kiswahili kwa hayo na mengine mengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *