
Muungano wa Walimu wa Nigeria umeitisha mgomo wa wazi kuanzia leo Jumatatu katika jimbo la Oyo kupinga kutekwa nyara makumi ya watoto na walimu wao katikati ya mwezi wa Mei mwaka huu.
Mnamo Mei 15, watu wenye silaha ambao jeshi la Nigeria liliwatuhumu kuwa magaidi wa kundi la kitakfiri la Boko Haram waliwateka nyara wanafunzi na wafanyakazi kutoka shule tatu katika jimbo la Oyo, kusini magharibi mwa Nigeria.
Mammala husika kaskazini mwa Nigeria zimeendelea kukabiliana na tatizo la utekaji nyara ili kulipwa fidia hata hivyo kitendo cha kuwateka nyara watu wengi si jambo la kawaida au lililozoeleka katika jimbo la Oyo. JImbo hilo ni kati ya majimbo yenye watu wengi nchini Nigeria.
Inafaa kuashiria hapa kuwa walimu saba walitekwa nyara pamoja na wanafunzi kati ya 25 na 39 wenye umri wa miaka miwili hadi 16 katika jimbo hilo tarehe 15 mwezi Mei mwaka huu.
Muungano wa Walimu wa Nigeria umewataka walimu wa shule za msingi na sekondari katika jimbo la Oyo kusitisha masomo kuanzia leo Jumatatu hadi itakapotolewa taraifa.
Muungano huo umesema kuwa mgomo huo umeitishwa kulalamikia na kupinga kutekwa nyara na kuendelea kushikiliwa walimu na wanafunzi bila sababu yoyote.