
Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kwamba vikosi vyake vimetekeleza mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya meli ya adui, makao makuu ya Kikosi cha Tano cha Jeshi la Wanamaji la Marekani nchini Bahrain, pamoja na kambi ya jeshi la anga ya Marekani katika eneo hilo, kufuatia vitendo viwili vya uchokozi wa Marekani vilivyolenga mali za Iran.
Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi yake ya Uhusiano wa Umma siku ya Jumatano, IRGC ilisema matukio hayo yalianza usiku wa manane wakati meli ya mafuta ya Iran ilipopigwa karibu na Mlango wa Hormuz.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, “Usiku wa jana, jeshi la Marekani lenye hulka ya uchokozi lilishambulia meli ya mafuta ya Iran kwa kombora la angani katika eneo la karibu na Mlango wa Hormuz, na kusababisha uharibifu katika chumba cha injini cha meli hiyo.”
IRGC ilisema tukio hilo lilisababisha jibu kutoka kwa vikosi vyake vya majini.
Jeshi hilo lilisema: “Kwa kujibu uchokozi huu na ukiukaji wa kanuni zinazosimamia Mlango wa Hormuz, meli ya mizigo ya adui wa Kimarekani-Kizayuni iitwacho Panaya ililengwa kwa makombora yaliyorushwa na Jeshi la Wanamaji la IRGC.”
Taarifa hiyo iliendelea kueleza kitendo cha pili cha uchokozi na kusema katika kitendo kingine cha uchokozi, jeshi la adui Mmarekani lililenga mnara wa mawasiliano wa IRGC katika sehemu ya kusini ya Kisiwa cha Qeshm kwa shambulizi la angani.”
IRGC imesema imetekeleza operesheni za kulipiza kisasi baada ya hujuma hiyo.
“Kwa kujibu uchokozi huu, kambi yao ya ndege na helikopta iliyoko katika moja ya nchi za eneo hili, pamoja na makao makuu ya Kikosi cha Tano cha Marekani, vilishambuliwa kwa makombora na ndege zisizo na rubani na Kikosi cha Anga za Juu cha IRGC.”
Jeshi hilo lilisema operesheni hizo za kujibu zilikuwa sambamba na maonyo yake ya awali.
“Tulikuwa tayari tumeonya kwamba kitendo chochote cha uchokozi kingekabiliwa na jibu tofauti na zito zaidi, na tumetenda ipasavyo. Majibu haya yanapaswa kuwa funzo.”
“Tunasisitiza tena kwamba kuvuruga usalama wa Mlango wa Hormuz kutaligharimu pakubwa jeshi la Marekani lenye hulka ya uchokozi.”
Iran ilikabiliana na duru ya hivi karibuni ya vita vya kichokozi vya Marekani na utawala wa Israel, vilivyoanza tarehe 28 Februari, kwa angalau mawimbi 100 ya mashambulizi ya kujibu yaliyoelezwa kwa mafanikio. Mashambulizi hayo yalilenga maeneo nyeti na ya kimkakati ya Marekani na Israel kote katika eneo la Asia Magharibi. Jamhuri ya Kiislamu pia iliufunga Mlango wa Hormuz kwa maadui na washirika wao.
Kufiatia jibu hilo kali la Iran, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kusitisha mapigano kwa upande mmoja tarehe 7 Aprili.
Jamhuri ya Kiislamu ilianza kuweka udhibiti mkali zaidi katika mlango wa Hormuz baada ya Trump kutangaza kuendelea kwa mzingiro wa kijeshi wa majini dhidi ya meli na bandari za Iran tarehe 13 Aprili, jambo lililoelezwa kuwa ni ukiukaji wa masharti ya kusitisha mapigano.
Ili kufanikisha usimamizi wa eneo hilo, Iran ilianzisha Mamlaka ya Mlango wa Ghuba ya Uajemi (PGSA), mfumo mpya wa kitaasisi wa kudhibiti na kusimamia usafiri wa vyombo kupitia njia hiyo muhimu ya baharini.