Tanzania imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini huku bei zake zikisalia kuwa nafuu zaidi ikilinganishwa na baadhi ya nchi jirani.

Kwa mujibu wa bei mpya zilizotangazwa na EWURA kuanzia leo Juni 3, 2026, petroli katika Mkoa wa Dar es Salaam itauzwa kwa shilingi 4,086 kwa lita, dizeli shilingi 4,333 na mafuta ya taa shilingi 4,685 kwa lita.

Petroli imepungua kwa zaidi ya shilingi 30 kwa lita ikilinganishwa na mwezi uliopita, huku dizeli ikiendelea kunufaika na ruzuku ya shilingi 535 kwa kila lita.

Licha ya changamoto zinazoikabili dunia kutokana na migogoro inayoendelea Mashariki ya Kati na athari zake katika biashara ya mafuta, Tanzania imeendelea kudhibiti ongezeko la bei na kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini.

Ruzuku ya dizeli imeendelea kusaidia sekta muhimu za uchumi ikiwemo usafirishaji, viwanda na kilimo, hatua inayochangia kupunguza gharama za uzalishaji na huduma kwa wananchi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *