Shirika la Afya Duniani (WHO) na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) vimetangaza mnamo Juni 5, 2026, uzinduzi wa mpango wa pamoja wa dola milioni 518 (euro milioni 446), unaoanza mwezi Juni hadi mwezi Novemba, ili kupambana na mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na nchi jirani.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Mpango huo unazingatia maeneo muhimu: uratibu wa dharura, ufuatiliaji, upimaji wa maabara, kinga na udhibiti wa maambukizi, huduma ya kliniki, na uhamasishaji wa jamii,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus katika mkutano na waandishi wa habari.

“Huu ni mpango thabiti. Unaelezea kile tunachopaswa kufanya hivi sasa, pamoja, ili kudhibiti mlipuko wa sasa na kupunguza hatari ya kuenea zaidi,” ameongeza.

Mlipuko huo ulitangazwa Mei 15 kaskazini mashariki mwa DRC, lakini mamlaka za afya zinashuku kwamba aina adimu ya virusi vya Ebola ya Bundibugyo ilikuwa ikisambaa bila kugundulika kwa muda fulani.

Kulingana na takwimu za hivi karibuni za WHO, wagonjwa 381 wamethibitishwa nchini DRC, ikiwa ni pamoja na vifo 64.

Mlipuko huo kaskazini mashariki mwa DRC, uliojikita katika mkoa wa Ituri ukiwa na 90% ya wagonjwa waliothibitishwa na 76% ya vifo, kulingana na Africa CDC, umeathiri mikoa mitatu.

Upande mwingine wa mpaka kuelekea kaskazini mashariki, nchini Uganda, wagonjwa 16 wamethibitishwa, ikiwa ni pamoja na kifo kimoja.

CDC inakadiria mlipuko wa sasa unaohusisha aina ya virusi vya Bundibugyo kuwa mkubwa kuliko ile miwili iliyopita, ambayo ilitokea mwaka wa 2007 na 2012.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *