PPRA YAONESHA UTAAYARI WA KUKABILIANA NA MAJANGA YA MOTO

Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) limefanya zoezi la kupima utayari wa kupambana na majanga ya moto, katika Ofisi zake za Makao Makuu jijini Dodoma, Mei 2, 2026.

Akizungumza baada ya zoezi hilo, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Dodoma SSF Rehema Menda amesema zoezi hilo limeonesha kuwa Mamlaka hiyo imejipanga kukabiliana na majanga ya moto.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za PPRA, Batholomeo Jungu, Ndc amewapongeza wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwa jinsi walivyochukua hatua za haraka katika kujiokoa na tishio la janga la moto.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *