
Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zimeongoza orodha ya kila mwaka ya Baraza la Wakimbizi la Norway (NRC) ya migogoro ya kibinadamu iliyopuuzwa zaidi duniani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na ripoti ya NRC iliyotolewa Alhamisi, nchi zote mbili zinaendelea kushuhudia viwango vikubwa vya vurugu,kuhama kwa watu wengi, na mahitaji makubwa ya kibinadamu, lakini zinapokea umakini na ufadhili mdogo wa kimataifa.
Nchini Sudan, mgogoro usioelezeka unaoendelea kati ya jeshi na wanamgambo kutoka Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) umewahamisha mamilioni ya watu na kusukuma sehemu kubwa ya watu kukaribi kukumbwa na njaa. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, vurugu zinazoendelea katika maeneo ya mashariki zimesababisha moja ya migogoro mikubwa zaidi duniani ya watukuhama makazi yao, ikiwa na mwitikio mdogo wa kimataifa.
NRC imebainisha kwamba migogoro hii inatokana na “kupuuzwa kwa muda mrefu” – ikipokea habari chache sana kutoka kwa vyombo vya habari na usaidizi wa wafadhili ikilinganishwa na dharura zingine za kimataifa. Ripoti hiyo imeonya kwamba ukosefu huu wa umakini unafaya mateso kuwa mabaya zaidi na kuongeza muda wa migogoro.
Katibu Mkuu wa NRC Jan Egeland amesema kwamba dunia inawaacha mamilioni ya watu walionaswa katika migogoro iliyosahaulika. Amezitaka serikali, wafadhili, na vyombo vya habari kuongeza mwonekano na usaidizi kwa dharura hizi zilizopuuzwa.