Katika kuendeleza ujumbe wa mshikamano wa kitaifa na siasa za kistaarabu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi, amevutia hisia za wananchi jijini Arusha baada ya kusimamisha msafara wake na kusalimiana pamoja na kufanya mazungumzo mafupi na wananchi waliokuwa katika moja ya vijiwe vya kisiasa, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu tofauti za kiitikadi kwa ajili ya kulinda amani na umoja wa Taifa.
Kihongosi amesema tofauti za kisiasa ni sehemu ya demokrasia, lakini hazipaswi kuwa chanzo cha migawanyiko miongoni mwa wananchi. Ameeleza kuwa ushindani wa kisiasa unapaswa kujengwa katika hoja, sera na maono ya maendeleo yatakayowanufaisha Watanzania wote.
Amehimiza viongozi na wananchi kuendelea kudumisha utamaduni wa kuheshimiana na kuvumiliana, akibainisha kuwa amani na mshikamano wa Taifa ndiyo msingi muhimu wa maendeleo endelevu ya Tanzania
(Feed generated with FetchRSS)