AFP

Chanzo cha picha, AFP

Jeshi
la Marekani limesema limedungua ndege nne zisizo na rubani za Iran zilizokuwa zikielekea
Mlango bahari wa Hormuz, na kudai kuwa yalikuwa tishio la moja kwa moja kwa
usafiri wa majini eneo hilo na mataifa mengine ya Ghuba ya Uajemi.

Kituo kikuu cha kuendesha oparesheni za
Marekani za Kijeshi (CENTCOM) imesema
kuwa baada ya kudungua ndege hizo, vikosi vya Marekani vilishambulia vituo vya
rada za ufuatiliaji vya Iran katika eneo la Goruk na Kisiwa cha Qeshm ili
kuzuia mashambulizi zaidi.

Iran ilijibu hatua ya
Marekani kwa kurusha makombora ya
balistiki na kulenga kambi za kijeshi za Marekani
zilizoko Kuwait na Bahrain.

CENTCOM
imesema kati ya
makombora saba ya Iran yaliyolenga nchi hizo mbili za Ghuba, sita yalidunguliwa
huku moja haikufikia lengo lake.

Pia unaweza kusoma:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *