
Biashara imesimama katika mpaka kati ya Uganda na DRC. Vizuizi vinavyohusiana na Ebola vinazuia malori na kusababisha bidhaa kuharibika. Wafanyabiashara wanasema wanapata hasara kubwa, huku mamlaka zikiimarisha hatua za kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola nchini Uganda.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kufungwa kwa mpaka kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na mlipuko wa Ebola kumesababisha usumbufu mkubwa wa biashara, na karibu malori 50 yanayobeba bidhaa yamekwama mpakani na kusababisha bidhaa mbalimbali ikiwa ni pmoja na chakula kuharibika.
Hali hii inaleta ugumu wa kiuchumi kwa wakulima na wachuuzi wa eneo hilo, na inazua mjadala kuhusu hitaji la kusawazisha afya ya umma na mambo muhimu ya biashara ya haraka, huku kukiwa na wasiwasi unaoongezeka kuhusu upatikanaji wa chakula na bei.
Hayo yanajiri wakati Shirika la afya Duniani (WHO) linaripoti karibu visa 500 vya Ebola katika mlipuko unaokua kwa kasi DRC na Uganda, huku vifo vikiongezeka ndani ya siku moja.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema karibu visa 500 vya Ebola vimethibitishwa katika mlipuko unaoendelea kushika kasi Afrika ya Kati, hali inayoongeza wasiwasi kuhusu ukubwa wa janga hilo.
Katika ripoti yake ya kila siku, WHO imethibitisha visa 452 na vifo 82 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku Uganda ikiripoti visa 19 na vifo viwili. Hii inaashiria ongezeko kubwa la zaidi ya visa 100 na vifo 20 ndani ya siku moja.
Maafisa wa afya wanaonya kuwa bila hatua za haraka za kudhibiti maambukizi, mlipuko huu unaweza kufikia kiwango kikubwa sawa na janga la Ebola la Afrika Magharibi mwaka 2014, ambalo liliua zaidi ya watu 11,000.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Ghebreyesus, anasema mlipuko unasonga kwa kasi na mataifa yanapaswa kuchukua hatua za haraka na kwa pamoja ili kuudhibiti kabla haujasambaa zaidi.