Kituo cha Nishati ya Nyuklia cha Bushehr nchini Iran ni miongoni mwa vituo 10 vya juu vya nyuklia duniani kwa upande wa usalama na ufanisi. Haya yamebainishwa na Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI).

Kulingana na Mohammad Eslami, Kituo cha Nguvu za Nyuklia cha Bushehr kimepata alama bora kwa miaka mitatu mfululizo.

“Hali ya kituo cha Bushehr ni bora, na imepata alama 100 kati ya 100 kwa mwaka wa tatu mtawalia,” ameeleza Eslami.

Ameeleza kuwa, kituo hicho cha nyuklia kimezalisha umeme wa zaidi ya kilowati bilioni 80.  

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa hatua hiyo muhimu ni ushahidi wa kutegemewa kwa kituo hicho cha nguvu za nyuklia na ni mchango wa muda mrefu katika sekta ya nishati nchini.

“Haya ni mafanikio makubwa ambayo yanadhihirisha kuwa inawezekana kusimama kidete na kutimiza ahadi katika hali yoyoye ile,” amebainisha Mohammad Eslami.

Mkuu wa AEOI amesema kuwa nishati ya nyuklia inayozalishwa huko Bushehr ni chanzo safi na endelevu cha umeme. Umeme wa nyuklia ni aina salama na thabiti ya nishati isiyotoa moshi.

Eslami amekadiria kuwa kiwanda hicho imezalisha akiba ya kiuchumi sawa na takriban dola bilioni 10 katika kipindi cha chini ya miaka 11, ikilinganishwa na uwekezaji wa awali wa karibu dola bilioni 1.87.

Amesema ujenzi wa kitengo cha 2 na 3cha Bushehr unaendelea kama kawaida licha ya vita dhidi ya Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *