Jumla ya miradi 63 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 50 katika wilaya saba na halmashauri tisa za Mkoa wa Morogoro inatarajiwa kupitiwa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Kighoma Malima, wakati akipokea Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Gairo ukitokea Mkoa wa Dodoma ambapo amesema ukaguzi huo unalenga kuangalia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuhakikisha thamani ya fedha za umma inaonekana kupitia huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Japhar Kubecha, amesema katika Wilaya ya Gairo pekee, Mwenge wa Uhuru utapitia, kukagua, kuweka mawe ya mIsingi miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni tisa katika Halmashauri ya Wilaya Gairo.

Miradi hiyo inagusa sekta mbalimbali muhimu za maendeleo na inatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika kuboresha huduma za kijamii na kuchochea maendeleo ya wananchi wa Wilaya hiyo.

Mwenge wa uhuru Kitaifa kwa mwaka 2026 unaongozwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Wazo Michael Mwang’onda.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *