
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 6
Siku mia moja zimepita tangu vita vilipozuka asubuhi ya Februari 28, 2026, na mashambulizi ya wakati mmoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran; vita vilivyolenga uongozi wa juu wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu kuanzia mwanzo na kuenea haraka hadi kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz, na nchi za Kiarabu katika eneo la Ghuba, na Lebanon.
Taarifa hii inaangazia matukio 10 muhimu za siku 100 za kwanza za vita.
Mbali na kiongozi huyo aliyekuwa na umei wa miaka 86, makamanda kadhaa wakuu wa kijeshi pia waliuawa katika mashambulizi hayo ya siku ya kwanza ya vita. Ali Shamkhani, Katibu wa Baraza la Kitaifa la Ulinzi, Abdulrahim Mousavi, Mkuu wa Majeshi, Mohammad Pakpour, Kamanda Mkuu wa Walinzi wa Mapinduzi, na Aziz Nasirzadeh, Waziri wa Ulinzi, walikuwa miongoni mwa watu muhimu zaidi waliouawa.
Tukio hili lilikuwa pigo kubwa zaidi katika muundo wa utawala wa Iran tangu kuasisiwa kwake, na kuanzia siku hiyo vita hivyo vilegeuka kuwa mzozo wa kikanda.
Kuanza kwa vita na kuuawa kwa Ali Khamenei
Alfajiri ya Jumamosi, Februari 28, 2026 Marekani na Israel zilifanya mashambulizi makubwa dhidi ya vituo vya kijeshi, usalama na kisiasa vya Iran.
Jeshi la Israel lilitangaza siku hiyo kwamba limeshambulia kwa wakati mmoja maeneo matatu ambapo wajumbe wa serikali ya Iran walikuwa wamekusanyika, na kwamba “vigogo kadhaa” wa serikali ya Iran “wameuawa” katika operesheni hiyo.
Baada ya saa 20, televisheni ya taifa ya Iran ilitangaza rasmi kifo cha Ali Khamenei.
Shambulio dhidi ya shule ya Munib
Shule ya msingi ya Minab, Mkoani Hormozgan, ililengwa siku ya kwanza ya vita.
Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu 156, wengi wao watoto wa shule wenye umri wa kati ya miaka 7 na 12. Walimu kadhaa na wazazi wa wanafunzi hao pia waliuawa katika shambulio hilo.
Maafisa wa Iran walizilaumu Marekani na Israel kwa kutekeleza shambulio hilo, na ripoti zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa zilieleza kuwa jeshi la Marekani lilihusika katika shambulio hilo, lakini Washington haijakubali rasmi kuhusika.
Shambulio hilo lilikosolewa vikalii ndani ya Marekani na pia kuzua hisia za kimataifa.
Chanzo cha picha, Getty Images
Kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz
Katika siku za kwanza za vita, Iran ilidhibiti vikali usafiri wa meli kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz, hatua ambayo iligeuza mkondo wa vita kutoka kwa makabiliano ya kijeshi na kuwa mgogoro wa nishati ya duniani.
Hatua hii ilikuja baada ya vitisho vya miaka mingi na, kwa mara ya kwanza hatua hiyo, iliruhusu Iran kudhibiri usafiri wa baharini kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz kujibu mashambulizi ya Marekani na Israel.
Mlango wa bahari wa Hormuz ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta na gesi duniani, na hatua ya Iran kuzuia meli kupitia hapo kumesababisha kuongezeka kwa bei ya mafuta, kuongezeka kwa gharama za bima ya meli, na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa meli katika Ghuba ya Uajemi.
Tangu wakati huo, kufunguliwa tena kwa njia hii ya kimkakati ya majini imekuwa lengo kuu la Marekani katika mazungumzo yaliyofuata, lakini sjku 100 baadaye, usafiri katika Mlango wa Hormuz bado haujarejea katika hali ya kabla ya vita.
Baadhi ya wachambuzi wanaamini kwamba vita vya siku 40 viliifanya Iran kutambua zaidi ya hapo awali umuhimu wa mkondo huu kama kichocheo kikuu cha shinikizo.
Kushambuliwa kwa kambi za jeshi la Marekani katika mataifa ya Ghuba
Katika wiki za kwanza za vita, Iran ilifanya mashambulizi makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel, pamoja na malengo kadhaa katika nchi za Kiarabu katika eneo hilo.
Bahrain, Kuwait, Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na Qatar ziliripoti kuzuia makombora na ndege zisizo na rubani au mashambulizi dhidi ya maeneo yanayohusiana na wanajeshi wa Marekani.
Baadaye, uchunguzi wa idara ya uchunguzi ya BBC Idhaa ya Kiajemi ulifichua kuwa wakati wa vita vya siku 40, Iran ilishambulia kambi 20 za jeshi la Marekani katika mataifa manane, ina huenda idadi halisi ya vituo vilivyoharibiwa inaweza kuwa kubwa zaidi.
Mashambulizi hayo yalisababisha uharibifu mkubwa kwa mitambo ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na rada za gharama kubwa na muhimu na ndege zilizowekwa kwenye vituo hivi.
Wakati huo huo, Marekani na Israel ziliendelea kushambulia malenge mengi ya kijeshi, hifadhi ya makombora, majini na usalama ndani ya Iran.
Katika kipindi hiki, hospitali kadhaa, vyuo vikuu, na vituo vya kiraia pia vililengwa au kuharibiwa katika mashambulizi, ikionyesha mwelekeo wa kibinadamu wa vita.
Chanzo cha picha, Getty Images
Mojtaba Khamenei: kiongozi wa tatu wa Iran
Mnamo tarehe 8 Machi, vyombo vya habari vya Iran vilitangaza kuwa Mojtaba, mtoto wa Ali Khamenei, ameteuliwa kuwa kiongozi mkuu mpya wa Jamhuri ya Kiislamu.
Kwa kuzingatia hali ya usalama na vita vilivyokuwa vikiendelea, hakuna taarifa nyingi zilizotolewa kuhusiana na muda wa kikao cha wataalamu kilichofikia uamuzi huo, na utaratibu uliotumika kumtambulisha mtoto wa kiongozi huyo wa zamani kuwa mrithi wa baba yake.
Uteuzi wa Mojtaba Khamenei ulikuwa ni moja wapo ya sehemu muhimu za mabadiliko ya kisiasa katika vita hivyo. Serikali ya Iran iliiwasilisha kama ishara ya kuendeleza utawala na kudumisha hali ya utulivu, lakini wakosoaji walisema uamuzi huo unaonyesha jinsi uongozi wa Jamhuri hiyo ya Kiislamu na IRGC unavyoelekezwa kwa watu wanaomzunguka kiongozi mkuu.
Kuuawa kwa Ali larijani
Mnamo Machi 17, Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na kiongozi mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Iran, aliuawa katika shambulio la Israel.
Kuuawa kwa Ali Larijani kulionyesha kuwa wigo wa mashambulizi hauko kwa makamanda wa kijeshi pekee, na kwamba viongozi wakuu wa kisiasa pia wako kwenye orodha ya wanaolengwa.
Kuuawa kwake pia kulionyesha hoja kwamba kumuondoa mtu aliyekuwa na jukumu muhimu katika kuunda taratibu za nje na pia za ndani za serikali kutoka kwa muundo wa mamlaka kungefanya maamuzi huko Tehran kuegemea kwenye nafasi ngumu zaidi.
Bwana Larijani aliuawa katika wakati na chini ya mazingira ambapo, bila ya Ali Khamenei, kiongozi wa zamani wa Jamhuri ya Kiislamu, na kisha kutokuwepo kwa kiongozi mpya, ilisemekana kwamba alikuwa “kiongozi” katika udhibiti wa masuala ya serikali.
Shambulio dhidi ya “daraja kuu Mashariki ya Kati” huko Karaj
Tarehe 2 Aprili, Daraja la B1 katika eneo la Bilqan mwanzoni mwa Barabara ya Chalus (Janbazan Boulevard) na Mto Karaj lilivamiwa na wanajeshi wa Marekani na kuharibiwa vibaya. Daraja hilo, ambalo lilipaswa kushikilia rekodi ya daraja “kubwa zaidi” katika eneo la Mashariki ya Kati, limekuwa mfano wa shambulio la miundombinu ya kiraia ya Iran.
Saa chache baada ya sehemu za daraja hilo kuporomoka, Rais wa Marekani Donald Trump alichapisha picha za daraja hilo likilengwa katika ujumbe kwenye Twitter, kuandika: “Daraja kubwa zaidi nchini Iran limeporomoka na halitatumika tena. Mengi zaidi yanakuja!”
Rais wa Marekani pia alionya: “Wakati umewadia kwa Iran kufikia makubaliano kabla mambo hayaharibika!”
Ingawa shambulio dhidi ya daraja hilo lilikabiliwa na athari nyingi, halikuwa shambulio la kwanza la miundombinu ya Iran. Hapo awali, Kiwanda cha Chuma na Isfahan, Kiwanda cha Chuma cha Mobarakeh huko Ahvaz, Kisiwa cha Kharg, na Uga wa Mafuta wa Pars Kusini zililengwa.
Wakati wa vita, mbali na kambi za kijeshi za Marekani, Iran pia ililenga maeneo ya kiraia katika eneo, vikiwemo viwanja vya ndege na vituo vya mafuta na petroli katika nchi za Ghuba ya Uajemi.
Tishio la Trump la “kuiangamiza Iran”
Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo Aprili 7, Donald Trump, katika moja ya kauli zake kali dhidi ya Iran, alionya kwamba ikiwa Tehran haitazingatia makubaliano, “itaangamizwa.”
Kauli hiyo ilikosolewa vikali kimataifa, huku mashirika ya kutetea haki za binadamu yakiitaja kuwa tishio la kutia hofu raia. Msimamo huu, pamoja na kuongezeka kwa shinikizo la kijeshi na kidiplomasia la Marekani, ulizua wasiwasi kuhusu wigo mpana wa vita.
Usitishaji mapigano
Siku moja baada ya vitisho vya Trump ambavyo havijawahi kushuhudiwa, Aprili 8, Iran na Marekani zilikubaliana kusitisha mapigano kwa muda.
Ingawa usitishaji huu wa mapigano ulisababisha kupungua kwa uhasama, makubaliano hayo yalikuwa dhaifu tangu mwanzo.
Mzozo kuhusu Mlango-Bahari wa Hormuz, kuendelea kwa mashambulio ya Israel huko Lebanon, na masharti ya makubaliano haya ya kusitisha mapigano yaliwafanya wahusika kupunguza kiwango cha makabiliano.
Katika wiki zilizofuata, pande hizo mbili zilituhumiana mara kwa mara kuhusu ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Chanzo cha picha, Getty Images