• Baba ya Zuhura Rama alimpa sifa Mbunge wa Msambweni Feisal Abdallah kwa kugharamia sehemu kubwa ya gharama zilizohusiana na mazishi ya binti yake
  • Baba huyo mwenye huzuni alisema Mike Sonko alichangia KSh 50,000 pekee kusaidia kulisha waombolezaji baada ya kukuta kwamba maandalizi mengi ya mazishi yalikuwa tayari yamekamilishwa
  • Mzee Rama alimkosoa Sonko kwa kutangaza msaada wake kwenye mitandao ya kijamii, akisema familia inaweza hata kumrudishia pesa hizo ikiwa alikuwa na nia nyingine nyuma ya msaada huo

Familia kumi na sita kote nchini bado zinaomboleza vifo vya kusikitisha vya mabinti wao waliopoteza maisha katika ajali ya moto wa bweni la shule ya Utumishi Girls Academy.

Rama Mohammed anamkashifu Mike Sonko kwa kujidai ambapo inadaiwa hakusaidia.
Babake Zuhura Mohamed alimkosoa Mike Sonko baada ya kumshika mkono wakati wa mazishi ya bintiye. Picha: Mike Sonko.
Source: Facebook

Mmoja wa wasichana hao, Zuhura Rama kutoka Kaunti ya Kwale, alizikwa hivi karibuni kwa mujibu wa mila za Kiislamu, huku familia za wasichana wengine 15 zikisubiri ibada ya pamoja ya kuwaenzi waliopoteza maisha, ambayo imepangwa na serikali.

Serikali iliahidi kuwapa wazazi walioathirika KSh 200,000 kusaidia kupunguza mzigo wa gharama za mazishi.

Pia soma

Eugene Mutuku: Familia ya Mwanafunzi wa KMTC Alibwagwa Nje ya Matatu Yalilia Haki

Kwa kuwa familia ya Zuhura ililazimika kumzika mara tu baada ya mchakato wa upimaji wa DNA kukamilika, walihitaji kupata rasilimali za kusafirisha mwili wake kutoka Naivasha hadi nyumbani na kugharamia mazishi huku wakisubiri msaada wa serikali.

Wakati maandalizi yalipokuwa yakiendelea, Mike Sonko aliingilia kati na kutoa msaada kwa familia hiyo.

Kama ilivyo kawaida yake, alishiriki taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii, akichapisha video kadhaa zikimuonyesha akiwasaidia wanafamilia waliokuwa kwenye maombolezo.

Hata hivyo, jambo hilo limezua mvutano na familia ya Zuhura, huku baba yake, Rama Mohammed, akimtuhumu aliyekuwa gavana wa Nairobi kwa “kujionyesha”.

Baba wa Kwale ampongeza Mbunge Feisal kwa msaada wa mazishi

Katika video moja, baba huyo mwenye huzuni alianza kwa kuishukuru serikali na viongozi wa eneo la Pwani kwa kumsaidia kumpa binti yake mazishi ya heshima.

Alieleza kuwa walipata msaada wa kuuchukua mwili kutoka Naivasha, huku usafiri ukiratibiwa na Mbunge wa Msambweni Feisal Abdallah.

“Feisal alilipia usafiri kutoka Naivasha hadi Mochari ya Coptic ya Nairobi iliyoko Ngong Road na kutoka hapo hadi uwanja wa ndege. Alituunga mkono kila hatua, na Sonko alifika tu tulipokuwa tayari mochari. Alikuta mchakato ukiendelea,” alisema Mzee Rama.

Pia soma

Utumishi Girl’s: Mmoja wa wasichana walioangamia katika mkasa wa moto azikwa Kwale

Kulingana na baba ya Zuhura, Sonko aliuliza kama walikuwa wanakabiliwa na changamoto yoyote, lakini walimweleza kuwa Mbunge Feisal tayari alikuwa ameshughulikia kila kitu na hawakuhitaji msaada mwingine.

Aliongeza kuwa mbunge huyo alilipa tiketi zote tano za ndege za familia kwenda Kwale, hivyo hawakuhitaji msaada wa kifedha zaidi.

Baba ya Zuhura Rama akosoa msaada wa Mike Sonko

Kwa mujibu wa Rama, alikubali mchango mdogo tu kutoka kwa aliyekuwa gavana huyo wa Nairobi ili kusaidia kulisha waombolezaji na wageni waliokuwa wakimiminika nyumbani kwake tangu kifo cha Zuhura.

“Nilimwambia atupatie kitu kidogo, lakini pia nilimhakikishia kwamba kwa kweli hatukuhitaji msaada wake. Hivyo ndivyo alivyotupatia KSh 50,000. Baadaye alileta gari lake kusaidia kusafirisha mwili, lakini nilikataa kwa sababu kila kitu tayari kilikuwa kimepangwa na kulipiwa na Mbunge Feisal,” alisema Rama.

Baba huyo mwenye majonzi alimkosoa Sonko kwa kutangaza msaada wake kwenye mitandao ya kijamii, akisema alikuwa anajipa sifa ambazo kwa hakika zilistahili kwenda kwa Mbunge Feisal.

Alimtaka aliyekuwa gavana huyo kuzungumzia tu msaada alioutoa yeye binafsi na asiiharibie jina mbunge huyo.

“Kama alitusaidia, ni kidogo tu, na tunamshukuru. Lakini kama alikuwa na nia mbaya katika kutusaidia, tunaweza hata kumrudishia pesa zake kwa sababu hapaswi kuharibu jina la mbunge wangu ambaye alitusaidia kwa dhati. Si vizuri kumsaidia mtu halafu ukaanza kujisifia. Ukimsaidia mtu kwa mkono mmoja, mwingine usijue,” alisema Rama.

Pia soma

Robai Agufa: Mfanyabiashara maarufu wa Vihiga akata roho ghafla akihudhuria mazishi ya rafiki yake

Mzee huyo aliendelea kusisitiza kwamba mbunge wake, na si mtu mwingine yeyote, ndiye aliyegharamia maandalizi yote ya mazishi.

Je, Mike Sonko alilipa tiketi za ndege za familia ya Zuhura?

Katika habari inayohusiana na hiyo, TUKO.co.ke iliripoti kwamba aliyekuwa gavana wa Nairobi alisema aliwasaidia wanafamilia wa msichana huyo waliokuwa wakisafiri kutoka Kijabe kupata pasi za kuabiria ndege.

Aliandamana na Mzee Rama pamoja na familia yote hadi uwanja wa ndege akiwa na msafara wa magari ili kuhakikisha wamepanda ndege yao salama.

Sonko alisisitiza kwamba alitoa msaada tu baada ya kuombwa kufanya hivyo na akapuuza madai kwamba alikuwa akijionyesha.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *