Benki ya NMB imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 230 katika teknolojia kwa kipindi cha miaka mitano (2021–2025) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wake mkakati wa kujenga benki imara, salama na yenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na vitisho vya wizi wa kimtandao.
Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, amesema uwekezaji huo umewezesha benki hiyo kuimarisha mifumo yake ya kidijitali na kuongeza ulinzi wa taarifa na miamala ya wateja, sambamba na kuboresha utoaji wa huduma za kifedha.
‘’Benki ya NMB imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 230 kwenye teknolojia, kwenye ujuzi wa watu wetu lakini pia ulinzi kuhakikisha kuwa tunakuwa Benki imara tunamlinda mteja wetu na benki kwa ujumla kutokana na uvamizi wa kimtandao’’
Mhariri | @rajjmsangi
#AzamTvUpdates
#MkutanoWa26WaWanahisaNMB

(Feed generated with FetchRSS)