Makao makuu ya taasisi yanayosimamia shughuli za kumuenzi shahidi Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, yametangaza kuwa shughuli ya kumuaga na mazishi ya Shahidi huyo yatafanyika baada ya siku 10 za mwanzo za mwezi wa Muharram.

Taarifa hiyo imesema kuwa mipango imefanywa kwa ajili ya shughuli za kumuenzi Shahidi Ayatullah Khamenei na watu wa familia yake ambao waliuawa shahidi katika hujuma ya kichokozi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa: Uvumi unaoenezwa katika vyombo vya habari vya ndani na nje kuhusu muda na namna mazishi yakakavyofanyika “hauna ukweli wowote” na umezua sintofahamu miongoni mwa watu wengi wanaotaka kuhudhuria tukio kuu la kitaifa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa: Uamuzi wa kufanya mazishi ya Ayatullah Khamenei na watu wa familia yake baada ya siku 10 za Muharram umechukuliwa kwa kuzingatia dhamira ya muda mrefu ya Kiongozi Muadhamu ya kufanya marasimu ya maombolezo ya Imam Hussein (AS), pamoja na umuhimu wa maombolezo ya Muharram ambayo hufanyika kote nchini Iran katika kipindi hicho kitakatifu. Mwezi Muharram unaanza Juni 16 mwaka huu.

Ayatullah Khamenei na watu kadhaa wa familia yake waliuawa shahidi katika hujuma ya kushtukiza ya siku ya kwanza ya mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel yaliyolenga makazi yake mjini Tehran, tarehe 28 Februari, wakati tawala hizo mbili za kigaidi zilipoanzisha vita vya kichokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *