Zuleikha Tambwe, ni Mtanzania ambaye amepata fursa ya kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya mkutano huu. Katika mazungumzo haya aliyoyafanya na Anold Kayanda wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Zuleikha anatathimini hatua zilizofikiwa katika kipindi cha miongo miwili ya mkataba.

Zuleikha Tambwe: Huu ni mkutano muhimu sana na tumejitahidi katika maandalizi na katika majadiliano yaliyoendelea kwa kiasi kikubwa. Malengo ya mkutano yamefanikiwa, utaona nchi wanachama nyingi zimeshiriki na nyingi zimeleta ujumbe kutoka makao makuu ya nchi zao, lakini kikubwa kilichofanikiwa ni jinsi ambavyo nchi zimekua zimeshiriki ya miaka ishirini ya tangu kuanzishwa kwa Mkataba wa Haki za Watu wenye ulemavu. Lakini lingine ni katika kubadilishana mawazo. Tumeangalia mafanikio yaliyopatikana njia bora za utekelezaji wa mkutano huo. Pia majadiliano Mengi yameangazia changamoto na mikakati ya jinsi ya kuitatua. Lakini kingine kikubwa na muhimu zaidi ni katika kuhamasisha Ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu kwa maana ya kwamba wapate nafasi ya kuchangia katika maeneo ya uchumi na kuleta maendeleo endelevu katika jamii yao.

Umetaja miaka ishirini hapo ya Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu miaka ishirini si michache. Ni kwa namna gani mkataba umefanikiwa duniani?

UN News/Feissal Kirwa Zuleikha Tambwe (kulia), Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mkutano wa 19, COSP19 akizungumza na Anold Kayanda (hayuko pichani) wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Juni 10, 2026.

Zuleikha Tambwe: Kwanza, mafanikio makubwa ya mkataba huu ni idadi ya nchi zilizoridhia mkataba. Mkataba huu wakati unapitishwa mwaka 2006 ulipitishwa na kuja kuanza kufanya kazi mwaka 2006 mwishoni wa uridhiaji. Nchi zilizoridhia zilikuwa ni chache, lakini mpaka sasa hivi tunapozungumza mkataba huo umeridhiwa na nchi 192. Ukitizama kwa haraka haraka utasema nchi ambazo ni wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa ujumla wake ni nchi 193 na kukosa mwanachama mmoja tu. Lakini mafanikio mengine yaliyopatikana ni kwamba mkataba huu ni kama nyenzo ya kusaidia nchi wanachama kuamua kuelezea ama kutekeleza haki za watu wenye ulemavu na upande huo. Sasa hii imesaidia nchi kuweka sheria kutengeneza sera, lakini pia kuunda taasisi zinazozingatia haki za watu wenye ulemavu. Hiyo ni sehemu moja lakini pia kingine kilichosaidia ni katika kutoa haki kwa watu wenye ulemavu. Maana yake sasa tuna shule. Elimu tu imeanza kuzingatia watu wenye mahitaji maalum lakini pia kwenye upande wa afya. Vile vile tunakuja kwenye upande wa miundombinu unapotaka kutengeneza barabara lazima uzingatie pia watu wenye mahitaji maalum watapita wapi, wataka wapi, lakini pia kwa maana ya majengo na vitu kama hivyo na nchi zinatekeleza na zinazingatia kingine, lakini ambacho pia ni kikubwa ni kuangalia jinsi ambavyo mkataba huu umesaidia kutoa elimu kwa familia zenye watu wenye ulemavu. Utaona zamani ni wakati wa kuwa na familia za karibu unaona kabisa na mtoto labda anapata ulemavu ama amezaliwa na ulemavu unaonekana labda ni bahati mbaya ni laana. Watoto hawa wanafichwa. Lakini siku hizi utaona watoto wanatolewa wanapelekwa shule, wanapelekwa maeneo ya kucheza. Kwa sababu elimu ya elimu imewafikia wahusika na watu wamehamasika na wanatekeleza. Kwa hiyo, nadhani mkataba umefanikiwa sana.

Haya ni mafanikio makubwa kwa vyovyote vile kuna changamoto hapa na pale unafikiri kuna jambo ambalo halijafanikiwa na ungependa kuiambia jumuiya ya kimataifa walifanyie kazi ili mambo mazuri zaidi yapo.

Zuleikha Tambwe: Ukiangalia kwenye kila mkataba hauwezi kuwa umetekelezwa kwa asilimia mia moja. Ziko changamoto hapa na pale. Changamoto ya kwanza ni katika teknolojia bado nchi zinazoendelea hazijaweza kupata teknolojia ya vifaa saidizi kwa watu wenye uhitaji. Lakini lingine ni suala la uwekezaji, bado nchi nyingi hazijaweza kuelekeza kiasi cha kutosha cha rasilimali katika kutekeleza mikakati iliyowekwa. Baadhi ya mikakati inabaki kwenye makaratasi, lakini lingine ni unyanyapaa ambao wakati mwingine utamwona mtu labda ana tatizo halafu jamii ikashindwa kumpokea kwa vile alivyo. Na lingine ambalo linafanyika japo sio kwa kiasi kikubwa ni ushirikishwaji. Tuna mikakati mingi mizuri inayoandaliwa, lakini haya yaandaliwe kwa ushirikishwaji wa watu wenye mahitaji yale. Muhimu ni kuwa na uandaaji wa sera na program. Ukiwa umewashirikisha watu wenye mahitaji ama umeshirikisha taasisi za watu wenye mahitaji hayo ili waweze kusema nini halisi wanahitaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *