Kuelekea siku ya uchangiaji damu duniani juni 14 mwaka huu Wilaya ya kigamboni kwa kushirikiana na Kikundi cha Maafisa usafirishaji wa Njia panda ya Nunge kilichopo Kata wa Vijibweni wilaya Kigamboni imeendesha zoezi la uchangiaji damu ili kufikia lengo la uhitaji wa damu Zaidi ya chupa 300 zinazohitajika ili kuokoa Maisha ya wahitaji wa damu.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuchangia damu katika kituo cha maafisa usafirishaji cha Njia panda ya Nunge mratibu wa huduma za maabara na damu salama wilaya ya kigamboni Marry Kauma amewataka wanachi wa wilaya ya kigamboni kujitolea kutoa damu kutokana na uhitaji mkubwa wa damu katika wilaya hiyo.

Zoezi la uchangiaji damu limefanyika kwa lengo la kuendelea kuunga mkono wizara ya Afya sambamba na jitihada za serikali katika kuhakikisha benki ya damu salama ya taifa inakuwa na akiba ya kutosha.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *