Ofisi ya Rais Ikulu imeandaa mafunzo kwa taasisi za umma huku taasisi za serikali 25 zikiwa zimearikwa kuhudhuria mafunzo hayo ambayo yanatolewa kwa siku 5 ndani ya mkoa wa Morogoro mafunzo hayo yanatolewa katika idara ya Utawala na rasilimari watu pamoja na idara za sheria

Akizungumza katika semina hiyo Katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro DKT Musa Ally Musa kwa niaba ya Katibu mkuu Ofisi ya Rais Ikulu Mululi Mahendeka amesema lengo la kuandaa semina hiyo ni kukumbushana na kueleweshana kuhusu uzingatiaji wa sheria kanuni na taratibu wakati wa utekelezaji wa majukumu yao

Kwa upande wake Mratibu wa mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Hilda Lugembe amesema kila mtu asimame kwenye nafasi yake ili kuweza kushughulikia masuala ya nidhamu na rufaa ili wasipate shida mbeleni

Naye katibu msaidizi Ofisi ya Rais, tume ya Utumishi wa umma Rose Silayo amesema watumishi wanapaswa kuzingatia maadili yaliyopo kwaajili ya sheria ambazo zimewekwa.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *