Mahakama nchini Nigeria imeamuru tume ya uchaguzi nchini humo, kufuta chama kikuu cha upinzani cha ADC kwenye kesi ambayo imeungwa mkono na mwanasheria mkuu wa serikali.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nigeria inaelekea uchaguzi mwezi Januari mwaka ujao, uchaguzi ambao rais Bola Tinubu atakuwa anatetea nafasi yake.

Hata hivyo miezi kadhaa mahama imeamuru kufutwa kwenye orodha vya vyama vitakavyoshiriki uchaguzi huu, chama cha ADC pamoja na vyama vingine vidogo, ikisema chama hicho hakijatimiza mahitaji ya kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Atiku Abubakar, mgombea wa urais kupitia chama cha ADC, akipinga uamuzi huo na kusema ADC itakataa rufaa akiitaja hatua hiyo kama ya kichochezi na pigo kwa demokrasia ya nchi.

Ikiwa Abubakar, makamu wa rais wa zamani,atafungiwa kuwania ,inamanisha kuwa uchaguzi huo hautakuwa na mgombea kutoka eneo la kaskazini ,na kulitenga eneo hilo kimaendeleo katika nchi ambapo uwakilishi wa kimaeneo kisiasa ni swala kubwa.

Kwenye uchaguzi wa mwaka 2023, Tinubu alipata asilimia 36.6 ya kura Abubakar akiwa kwenye nafasi ya pili akiwa na asilimia 29 ya kura zote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *