Kama ishara ya wasiwasi kuhusu mlipuko wa virusi vya Ebola nchini DRC, Umoja wa Afrika umeitisha mkutano kwa njia ya video siku ya Jumanne na wakuu wa nchi na mawaziri zaidi ya kumi kutoka kote barani Afrika ili kujaribu kukusanya fedha zaidi za kupambana na mlipuko huo. Kufuatia mkutano huo, mkurugenzi mkuu Kituo cha Kupambana na Kuzuia Magonjwa, Africa CDC, Jean Kaseya, aliiambia RFI kwamba amepata ahadi za jumla ya dola milioni 910.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Ni mwitikio wa pamoja na wa kipekee unaoweza kushinda ugonjwa huuu,” alisema Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. “Lazima tuchukue hatua haraka na kwa umoja,” aliongeza, akitoa wito kwa serikali za Afrika kubadilisha ahadi zao za michango kuwa rasilimali za haraka.

“Afrika lazima pia ionyeshe uongozi kwa kukusanya angalau dola milioni 100 kutoka kwa serikali za Afrika na sekta binafsi za Afrika, na hivyo kuonyesha uhuru wetu, uwajibikaji na mshikamano,” alisema rais wa Burundi.

Majibu ya dharura dhidi ya magonjwa ya mlipuko yanachochea mzunguko wa kudumu, alisema Mahmoud Ali Yussuf, mwenyekiti wa Tume ya AU, ambaye alitoa wito kwa bara hilo kuwekeza ili kukabiliana na majanga yanayoikabili Afrika.

“Tupambane vita hivi sisi wenyewe”

“Bara letu lina taasisi na maabara za utafiti za kiwango cha dunia: BioVac nchini Afrika Kusini, Taasisi ya Pasteur nchini Senegal. Tuna viwanda vya dawa vinavyofanya kazi vizuri barani. Tuna uhakika kwamba Big Pharma si lazima iwekeze katika utafiti ambao hauwaletei faida kubwa, kwa hivyo ni lazima tupigane vita hivi sisi wenyewe,” alisisitiza.

Mkurugenzi wa Africa CDC, shirika la afya la Umoja wa Afriia, AU, alionya: “Tusipozuia haraka kuenea kwaugonjwa huu,” Jean Kaseya alionya, “kuna hatari ya ugonjwa hu kuwa moja ya hatari kubwa zaidi barani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *