Marekani inatarajiwa kuiruhusu Iran kuanza kuuza tena mafuta yake, ikiwa ni sehemu ya mkataba wa amani wa kusitisha vita kwa siku 60 unaotarajiwa kusainiwa Ijumaa hii.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa gazeti la Wall Street Journal, Iran itaruhusiwa kuuza mafuta yake tena iwapo itazingatia masharti ya mkataba huo wa amani, ikiwemo kufungua njia ya bahari ya Hormuz na kuachana na mipango ya kuunda silaha za nyuklia.

Hatua hiyo huenda ikaibua mgawanyiko miongoni mwa washirika wa Iran pindi mkataba huo utakapowekwa wazi.

Hatua hiyo inajiri wakati bei ya mafuta katika soko la kimataifa ikiendelea kushuka na kufikia dola 80 kwa pipa kwa mara ya kwanza tangu mwezi Machi.

Mkataba huo wa amani kati ya Marekani na Iran unatarajiwa kusainiwa Ijumaa nchini Uswisi, hatua itakayotoa nafasi ya kuanza kwa mazungumzo zaidi ya kutafuta suluhu la kudumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *