Taasisi ya nchi wanachama wa Ushoroba wa Kati (Central Corridor) imeonesha nia ya kushirikiana na Bandari Kavu ya Bravo katika kuendeleza maeneo waliyopewa na Serikali katika eneo la Bandari Kavu ya Kwala.

Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo amesema hayo wakati wa ziara yao katika bandari hiyo kwa lengo la kujionea shughuli za uendeshaji wake, pamoja na kujifunza namna inavyorahisisha usafirishaji wa mizigo kwenda katika nchi wanachama wa Ushoroba wa Kati.

Amesisitiza kuwa uwepo wa maeneo hayo unasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza muda na gharama za usafirishaji wa mizigo, jambo linalochochea biashara na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi miongoni mwa nchi hizo.

Mhariri | @rajjmsangi

#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *