Katika taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi, WHO inasema huduma za mapema za usaidizi zinaweza kuokoa maisha ya watu wengi, hasa kwa kuwa bado hakuna chanjo au tiba zilizoidhinishwa kwa virusi vya Marburg na baadhi ya aina za ugonjwa wa Ebola

Magonjwa hayo mawili yamesababisha milipuko 72 barani Afrika tangu mwaka 1967 na kiwango cha vifo kinaweza kufikia asilimia 90 katika baadhi ya milipuko.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema, “Mlipuko wa sasa wa virusi vya Bundibugyo ni ukumbusho wa umuhimu wa huduma za kitabibu zilizo makini, jumuishi na zinazomweka mgonjwa katikati ili kuokoa maisha na kuhifadhi utu wa binadamu.”

Mapendekezo ya mwongozo mpya wa WHO

Mwongozo huo una mapendekezo 16 ya kisayansi kwa wahudumu wa afya, yakiwemo,

  • Kutumia vipimo vya maabara kufuatilia wagonjwa na kugundua matatizo yanayoweza kutibika mapema.
  • Kutibu haraka upungufu wa maji mwilini kwa kutumia maji ya kunywa na ya mishipa.
  • Kutumia maji yanayoongezwa kwa njia ya mishipa na dawa za kutibu mshtuko wa mwili kwa wakati muafaka.
  • Kuanza tiba ya viuavijasumu pale maambukizi ya bakteria yanapobainika.
  • Kutoa huduma za ufuatiliaji kwa manusura ili kuboresha afya na kuzuia maambukizi zaidi.

WHO inazitaka serikali na mamlaka za afya kujumuisha mwongozo huo katika maandalizi na hatua za kupambana na milipuko ili kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma bora na zinazookoa maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *