Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu amesema wanajeshi wa nchi yake wataendelea kusalia nchini Lebanon kwa kipindi kirefu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Netanyahu, wapiganaji wa Hezbollah watalipia gharama kubwa dhidi ya mashambulio yao dhidi ya wanajeshi wa Israeli au katika ardhi ya Israeli.

 “Israel haitokubali mashambulio dhidi ya wanajeshi wetu au katika ardhi yetu na Hezbollah italipia gharama kubwa kwa mashambulio hayo.” Amesema Benjamin Netanyahu.

“Israel itasalia katika maeneo ya kiusalama kusini mwa Lebanon kwa kipindi kirefu kwa lengo la kuzilinda jamii zetu za kaskazini.” Amesisitiza Netanyahu.

Naye Waziri wa ulinzi wa Israeli, Israel Katz ametangaza kuwa wanajeshi wa Israeli watasalia nchini Lebanon na kwamba watajibu kwa nguvu kubwa iwapo watashambuliwa.

Mwenzake wa usalama wa kitaifa wa Israeli Ben Gvir Waziri wa usalama wa kitaifa nchini Israeli Itamar Ben-Gvir amesema ni ‘lazima Lebanon yote iteketee’ kauli yake ikijiri baada ya wanajeshi wanne wa Israeli kuuawa kusini mwa nchi hiyo katika makabiliano na kundi la Hezbollah.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *