Mapigano yameripotiwa kuzuka tena nchini Lebanon, mamlaka ikithibitisha kuuawa kwa watu 18 wakati Israeli nayo ikiripoti kuuawa kwa wanajeshi wake wanne.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Makabiliano hayo ndio mbaya zaidi kuripotiwa tangu makubaliano ya Marekani na Iran kusitisha mapigano mashariki ya kati.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, makabiliano yote yalistahili kusitishwa, ikiwemo vita dhidi ya Israeli na Hezbollah huko Lebanon.
Mauaji ya wanajeshi hao wa Israeli yamekashifiwa vikali, Waziri wa ulinzi wa Israeli kutoka mrengo wa kulia Itamar Ben Gvirj, akisema “Lebanon ni lazima iteketee.”
Wizara ya afya ya Lebanon imethibitisha kuuawa kwa watu 18 kwenye mashambulio ya Israeli wakati 33 wakijeruhiwa.
Jeshi la Israeli limesema limeshambulia zaidi ya maeneo 80 za wapiganaji wa Hezbollah kusini mwa Lebanon na kusababisha mauaji ya wapiganaji kadhaa wa kundi hilo.
Nao wapiganaji wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran wamesema wameshambulia wanajeshi wa Israeli kusini mwa Mji wa Nabatieh nchini Lebanon.