Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesifu hati ya makubaliano ya Islamabad iliyotiwa saini kati ya Iran na Marekani kuwa ni “hati ya kihistoria” na dhihirisho la nguvu ya Iran duniani.

“Hii ni hati ya kihistoria na ujumbe kutoka kwa Iran yenye nguvu: Amani itapatikana katika kivuli cha kuheshimiana,” Pezeshkian ameandika kwenye mtandao wa kijamii siku ya Alhamisi, sambamba na kuonyesha picha za makubaliano yaliyotiwa saini.

Rais wa Iran amesisitiza kuwa azma thabiti ya Iran ya kudumisha amani duniani sambamba na ikilinda heshima yake, uhuru na maslahi ya taifa.

Amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran siku zote imekuwa ikiwajibika kwa dhati na kufanya jitihada za kuduumisha amani duniani, na kuunga mkono ustawi na ushirikiano wa kikanda.

Hati hiyo yenye vipengee 14 imetiwa saini kwa njia ya kidijitali na Marais Masoud Pezeshkian wa Iran na Donald Trump wa Marekani.

Wakati hyuo huo msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amefafanua kwamba uamuzi wa kufanya makubaliano hayo, yajulikanayo kama Mapatano ya Islamabad, yatiwe saini na viongozi wa juu kabisa wa nchi zote mbili umefanywa kwa makusudi kutokana na uzoefu wa nyuma.

Esmaeil Baghaei amesema kuwa taasisi za diplomasia za Iran, kwa kuungwa mkono kikamilifu na wananchi, zimefanikisha makubaliano yanayolinda maslahi ya taifa.

Amesisitiza pia kuwa Iran haitasita kujibu iwapo Marekani haitatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *