Chanzo cha picha, Getty Images
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3
Tottenham Hotspur ni klabu ya hivi karibuni kuonyesha nia ya kumsajili Adam Wharton. Liverpool bado hawajafikia makubaliano ya kumsajili Yan Diomande huku Fulham wakikosa kufanikiwa katika ofa yao ya kwanza kwa Chibuike Nwaiwu.
Tottenham Hotspur wako tayari kujaribu bahati yao kwa kutoa ofa kwa ajili ya kiungo wa kati wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Adam Wharton, mwenye umri wa miaka 22. (Teamtalk)
Chanzo cha picha, Getty Images
RB Leipzig wamekataa ofa ya pauni milioni 87 kutoka Liverpool kwa ajili ya winga wa Ivory Coast, Yan Diomande, mwenye umri wa miaka 19, kwani wanahitaji pauni milioni 113 ili kumuuza mchezaji huyo. (Liverpool Echo)
Chanzo cha picha, Getty Images
Ofa ya pauni milioni 17 ya Fulham yakataliwa na klabu ya Uturuki ya Trabzonspor kwa ajili ya beki wa Nigeria, Chibuike Nwaiwu, mwenye umri wa miaka 22. (Fotomac)
Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham hawana mpango wa kumsajili mshambuliaji Mason Greenwood kwa sasa, huku AS Roma wakishindwa kufikia kiwango cha fedha kinachohitajika na Olympique de Marseille kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Mail)
Everton, Tottenham Hotspur, na klabu mpya iliyopanda daraja ya Ipswich zafukuzia kumsajili mshambuliaji wa Cameroon mwenye umri wa miaka 22, Karl Etta Eyong, kutoka Levante UD msimu huu wa joto. (Teamtalk)
Chanzo cha picha, SNS
Celtic walikataa ofa ya pauni milioni 25 kutoka Nottingham Forest mnamo mwezi Januari kwa ajili ya kiungo wa kati wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 22, Arne Engels.
Hata hivyo, sasa wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya mchezaji huyo, huku Crystal Palace na Borussia Dortmund nazo zikionyesha nia ya kutaka kumsajili. (Football Insider)
Chanzo cha picha, Shutterstock
Klabu ya Leeds United inaonyesha nia ya kumtafuta kiungo wa Shea Charles kutoka Southampton msimu huu wa joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya pauni milioni 20.
Leeds pia inafuatilia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Julian Brandt, mwenye umri wa miaka 30, ambaye anapatikana bila ada ya usajili baada ya kuondoka Borussia Dortmund. (Yorkshire Evening Post)
Chanzo cha picha, Getty Images
Na, Wolverhampton Wanderers wanapanga kumrudisha mshambuliaji wa Scotland Che Adams kutoka klabu ya Italia Torino katika dirisha hili la usajili. (Tuttomercato – in Italian)