
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye anafanya ziara ya siku mbili nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ziara ya rais Ndayishimiye inakuja wakati huu akiwa pia Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Burundi na DRC zina uhusiano na ushirikiano mzuri chini ya viongozi hao wawili.
Miongoni mwa mambo ambayo yanajadiliwa kwenye mkutano wa rais Tshisekedi na Ndayishimiye ni kuhusu hali ya usalama Mashariki mwa DRC lakini pia mapambano dhidi ya virusi vya Ebola.
Ndayishimiye ambaye ni mshirika wa karibu na mwandani wa Tshisekedi kwenye ukandan, ametuma vikosi vya wanajeshi wa Burundi wapapatao 10,000 katika eneo la Minembwe jimboni Kivu Kusini kusaidiana na vikosi vya DRC kuwakabilia waasi wa Red Tabara.
Aidha, katika nafasi yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika rais Ndayishimiye pia anatulia ziara hii nchini kushauriana na wadau mbalimbali ikiwemo wakuu wa Monusco kuhusu juhudi za kuleta amani na utulivu katika maeneo ya mashariki mwa DRC, na maeneo mengine yenye migogoro kwneye eneo la Maziwa makuu.