
Watu 11 wamewauwa kwenye mashambulio mawili ya wanajihadi kaskazini mwa Nigeria, mwishoni mwa wiki iliopita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa taarifa kutoka wapiganaji wanaosaidiana jeshi kupambana na makundi yenye silaha, wanajihadi waliwashambulia na kuwauwa wakulima 7 katika kijiji cha Kuwawu jimbo la Borno kwa kuwachoma visu,wakati walikuwa wanaendela na shughuli za upanzi kwenye mashamba yao.
Miili ya wakulima hao saba ilipatikana jana Jumapili na kuzikwa.
Mapema kundi lingine la wanajihadi waliwauwa wakulima wanne kwenye mashamba yao eneo la Kross Kauwa ,eneo la ziwa Chad,wakiwa pia kwenye mashamba yao.
Kundi hilo linalopambana na wanajihadi limesema wanajihadi wa ISWAP ndio walihusika kwenye mauaji hayo.
Jamii zinazoishi kaskazini na eneo la kati nchini Nigeria, zimekuwa zikishambuliwa na wanajihadi na wahalifu wengine, ambao wanawatoza ada ili kutumia mashambo yao, wengine wakilazimika kulipa kiasi kikubwa ili kuachiwa kwa wapendwa wao ambao wametekwa.