
Wapatanishi Pakistan na Qatar wanasema Marekani na Iran zimefanya “maendeleo ya kutia moyo” katika siku ya kwanza ya mazungumzo ya ngazi ya juu nchini Uswisi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wanasema Marekani na Iran zimekubaliana kuhusu “ramani ya kufikia makubaliano ya mwisho ndani ya siku 60”, pamoja na “kitengo cha kuondoa migogoro” ili kuhakikisha mwisho wa “shughuli za kijeshi nchini Lebanon“.
Mazungumzo kati ya Iran na Marekani yenye lengo la kukomesha vita vya Mashariki ya Kati, yameendelea usiku wa kuamkia Jumatatu licha ya kuwa hatarini kuvunjika.
Siku ya Jumapili, ujumbe wa Iran uliondoka katika ukumbi wa majadiliano baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kuishambulia Iran kwa kuiunga mkono Hezbollah.