• Ruto na Gideon Moi walimaliza miaka ya uhasama wa kisiasa Oktoba mwaka jana, wakifunga makubaliano yaliyoifanya KANU kuungana na Kenya Kwanza pamoja na ODM
  • Rais alisifu muungano huo kama hatua ya mageuzi makubwa, akiahidi maendeleo katika kaunti ya Baringo huku Gideon akijiondoa kwenye mbio za useneta
  • Hata hivyo, miezi minane baadaye, makubaliano hayo yalivurugika, huku Ruto akimshambulia Gideon kupitia X, akimtuhumu kwa ulafi na kutumia Gazeti la The Standard kuishinikiza serikali yake

Oktoba mwaka jana, Rais William Ruto na mwenyekiti wa kitaifa wa KANU, Gideon Moi, walizika tofauti zao za kisiasa baada ya muda mrefu wa uhasama.

Rais William Ruto akiwa na Gideon Moi.
Rais William Ruto alisema KANU, chini ya Gideon Moi, itatia saini mkataba rasmi na serikali ya Kenya Kwanza. Picha: Gideon Moi.
Source: Twitter

Mnamo Oktoba 9, 2025, wawili hao walikutana katika Ikulu ya Nairobi na baadaye nyumbani kwa Gideon huko Baringo.

Ruto alitangaza kuwa alikuwa amemwalika Gideon kujiunga na serikali yake, akisisitiza kuwa maendeleo ya Kenya yanategemea juhudi za pamoja zinazovuka mipaka ya kisiasa.

Ili kusisitiza hoja yake, rais alisema tayari alikuwa ameshirikiana na Raila Odinga pamoja na rais mstaafu Uhuru Kenyatta, na sasa alikuwa akimkaribisha Gideon kushirikiana naye katika kuisukuma nchi mbele.

Pia soma

“Hajibu Kelele”: Video ya Tash Akionekana Mtulivu Licha ya Vinjembe vya Mitandaoni Yazuka

Kutokana na hilo, KANU chini ya uongozi wa Gideon ilikubali kushirikiana na serikali ya Kenya Kwanza, ikijiunga na ODM ambayo hapo awali ilikuwa imesaini makubaliano ya ushirikiano na UDA.

Ruto alisifu hatua hiyo kama njia ya kuibadilisha Kenya, akilinganisha uwezo wa nchi hiyo na ule wa Singapore, ambayo alisema wakati mmoja ilikuwa katika hali sawa na Kenya.

Alisisitiza kuwa maendeleo yanahitaji uungwaji mkono mpana na nia njema kutoka kwa wadau mbalimbali, na akaikaribisha KANU kushiriki katika kushughulikia changamoto za kitaifa.

Rais pia alijaribu kuwahakikishia wanachama wa KANU ambao walihisi kushitushwa na mpango huo.

Alieleza kuwa alimwomba Gideon kuandaa kongamano la viongozi wa mashinani katika eneo atakalochagua, ambalo baadaye lilikuwa Kabarak — mahali ambapo Ruto alisema lina umuhimu wa kipekee kwake binafsi kutokana na uhusiano wake wa awali wa kisiasa na marehemu Rais Daniel arap Moi.

Alidokeza uwezekano wa makubaliano rasmi kati ya Kenya Kwanza na KANU, akiwahimiza wanachama wa chama hicho kuukumbatia ushirikiano huo.

Ruto alitumia hafla hiyo kuahidi miradi ya maendeleo kwa Baringo, ikiwemo ujenzi wa uwanja wa michezo na chuo kikuu mjini Kabarnet.

Moja ya matokeo makubwa ya muungano wake na Gideon ilikuwa hatua ya Moi kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha useneta wa Baringo.

Pia soma

DJ Dizzo Afariki Dunia, Mlezi Wake DJ Kamjo Amuenzi Katika Ujumbe wa Kugusa Moyo

Hata hivyo, miezi minane baadaye, ushirikiano ambao Ruto alikuwa ameufurahia ulionekana kukumbwa na changamoto.

Katika ujumbe mkali aliomwelekeza Gideon kupitia mtandao wa X Jumatano, Juni 24, rais alifichua kuwa ulafi ulikuwa umeharibu makubaliano yao ya Oktoba.

Ruto alidokeza kuwa alikuwa tayari kutekeleza upande wake wa makubaliano hayo kama si ulafi ambao anadai ulikuwa upande wa seneta huyo wa zamani.

Rais alimshambulia Gideon kupitia madai yaliyolenga Standard Group, ambayo gazeti lake limekuwa likichapisha vichwa vya habari vinavyoikosoa serikali ya sasa.

Kwa mujibu wa Ruto, gazeti hilo limekuwa likitumika makusudi kama chombo cha kumshinikiza kisiasa, jambo ambalo alisema hatalikubali.

Alieleza kuwa Gideon ametumia gazeti hilo kama silaha ya kumlazimisha akubali matakwa ambayo hakuyafichua hadharani.

“GMoi, vichwa vya habari vya propaganda vya kulaghai na kunishinikiza vinavyochapishwa na vyombo vyako vya habari vya STANDARD siku 5 kwa wiki dhidi yangu na rekodi ya mageuzi ya utawala wangu havitakuletea CHOCHOTE wala KUKUPELEKA POPOTE. KUNISHINIKIZA ili nikubali ULAFI wako? KAMWE. Kenya ni ya Wakenya wote, si yako peke yako. Jaribu siku 8 kwa wiki. Fanya LOLUTE UWEZALO,” ilisoma taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya X ya Ruto.

Pia soma

Ruto Amrushia Gachagua Makombora Mazito Katika Hotuba Moto: “Inaonekana Hunijui”

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *