Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Idara ya WHO ya Virusi Vya UKIMWI, TB, Homa ya Ini na Maambukizi yanayosababishwa na Ngono, chanjo hizo mpya zinatarajiwa kuanza kuidhinishwa rasmi mapema mwaka 2029 kulingana na matokeo ya majaribio ya kitabibu, jambo linaloweza kuleta mapinduzi makubwa dhidi ya ugonjwa huo unaoongoza kwa kuua watu wengi duniani.

TB bado ni changamoto kubwa barani Afrika

Kaimu Mwakilishi wa WHO nchini Kenya, Dkt. Neema Rusibamayila Kimambo, akifungua warsha hiyo, amesema,“Kifua Kikuu bado ni changamoto kubwa sana barani Afrika, ambapo inasababisha karibu watu milioni 2.5 kuugua na vifo zaidi ya 400,000 kila mwaka. Kenya inajivunia kushiriki katika majaribio ya hatua za mwisho za chanjo mpya za TB kwa ajili ya watu wazima na vijana, na itakuwa moja ya nchi za kwanza kuzitumia katika ukanda huu.”

Dkt. Kimambo ameongeza kuwa kenya inajivunia kuwa mwenyeji wa mkutano huo. 

WHO inakadiria kuwa, ndani ya miaka 25, chanjo yenye uwezo wa kufanya kazi kwa asilimia 50 inaweza kuzuia hadi wagonjwa wapya milioni 76 wa TB, vifo milioni 8.5, na kuokoa dola za Marekani bilioni 6.5 ambazo zingetumiwa na familia zilizoathirika vibaya, hasa masikini.

Misingi ya kisheria na ushirikiano wa kijamii katika kufanikisha chanjo mpya

Katika warsha hiyo, washiriki wamejadili mambo yanayohitajika ili kufanikisha uingizaji wa chanjo hizo, kila nchi imeanza kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji ikiwa ni pamoja na kuunda vikundi maalumu vya kitaalamu vitakavyounganisha wadau wa ngazi mbalimbali, ikiwemo bunge, vyombo vingine vya kutoa maamuzi, mashirika ya kiraia, na jumuiya za kidini ili kujenga utayari wa kisiasa na kupata fedha endelevu za ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *