Wanajeshi wa Marekani kwa siku ya tano, wametekeleza mashambulizi kulenga miundo mbinu ya ulinzi ya Iran na makombora yao, na kuzuia kuendelea kwa shughuli zote kwenye bandari zake.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Iran nayo imeendeleza kulipiza kisasi kwa kulenga Kambi za wanajeshi wa Marekani katika nchi za Kuwait na Jordan.
Jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya Iran, linasema nchini Jordan kwa kutumia ndege zake zisizokuwa na rubani, limeshambulia mitambo ya mawasiliano ya jeshi la Marekani lakini pia eneo la kuhifadhi mafuta.
Wanajeshi wa Marekani nao wanasema, wameharibu meli ya mafuta ya Iran iliyokuwa kwenye eneo la Bahari la Hormuz.
Mashambulizi haya mapya kati ya Marekani na Iran yalianza wiki iliyopita, na kusababisha kuvunjika kwa mkataba wa kusitisha vita, huku kila upande ukitaka kudhibiti eneo la mlango wa Bahari la Hormuz.
Rais Donald Trump ameendelea kusisitiza kuwa mashambulizi hayo yataendelea hadi pale Iran itakapokubali kurejea kwenye meza ya mazungumzo.