Nchi ya Ufaransa hivi leo imetangaza kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Ebola, aliyegundulika ni daktari aliyerejea kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo inapambana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kisa hicho ni cha kwanza kuwahi kugundulika nchini Ufaransa lakini na cha kwanza kuripotiwa nje ya bara la Afrika katika mlipuko huu mpya wa ebola ambao pia umeathiri nchi ya Uganda.

Wizara ya afya ya Ufaransa imesema katika taarifa kwamba daktari huyo alitengwa punde baada ya kuwasili nchini humo, huku ofisi ya Waziri mkuu Sebastien Lecornu ikisema kuwa inafuatilia hali kwa ukaribu sana.

Mwaka wa 2014, mlipuko wa ebola uliposhuhudiwa katika eneo la Afrika Magharibi, wagonjwa wawili walisafirishwa nchini Ufaransa lakini walikuwa tayari wamegundulika kuwa na maambukizi hayo.

Hata hivyo watalam wa afya ya uma wanakadiria kwamba bado kuna hatari ndogo ya  mlipuko wa sasa kuenea duniani.

Mlipuko wa hivi punde ambao ni wa 17 kuripotiwa nchini DRC ulitangazwa mnamo mei 15 baada ya kuripotiwa vifo kadhaa katika jimbo la Ituri amchani ni kitovu cha mlipuko wa ugonjwa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *