Shughuli za umma na zile za binafsi nchini Kenya, hivi leo zinatarajiwa kutatizika katika baadhi ya maeneo kufuatia wito wa maandamano ya amani kuadhimisha kumbukizi ya vijana wa Gen Z waliouawa wakati wa maandamano ya mwaka 2024.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakati huu shughuli zikitarajiwa kutatizika, kumekuwa na wasiwasi wa kutokea vurugu wakati wa maandamano hayo, kutokana na hofu kuwa huenda baadhi ya makundi ya vijana wanaodaiwa kusailiwa na serikali wakatumia nafasi hii kuzua vurugu.

Hata hivyo waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Kipchumba Murkomen, amewahakikishia usalama raia watakaoandamana kwa amani huku akionya dhidi ya wale wanaopanda kufadhili vurugu.

Kauli yake imekuja wakati huu Serikali na baadhi ya wanasiasa wakinyooshewa kidole kufadhili makundi ya vijana wenye silaha kupiga raia pamoja na kutoa vitisho.

Aidha mashirika ya kiraia pamoja na wahanga wa vurugu za miaka miwili iliyopita, wameonya polisi na vijana wanaopanga kuharibu maandamano yao. Lavani Mila ni mmoja wa waathiriwa wa vurugu za mwaka 2024.

Licha ya serikali kuahidi shughuli kuendelea kama kawaida hivi leo, baadhi ya barabara kuu za kuingia jijini Nairobi zimefungwa, raia wakilazimika kurejea walikotoka.

Wakati wa maandamano ya mwaka 2024 kupinga serikali na muswada tata wa fedha, zaidi ya watu 60 wengi wao kwa majeraha ya risasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *