
Urusi inazidi kuimarisha udhibiti wake dhidi ya wakosoaji wake. Mwanzoni mwa mwezi Juni, Wizara ya Sheria ya Urusi ililiweka shirika lisilo la kiserikali la OVD-Info kwenye orodha yake ya mashirika yenye msimamo mkali bila sababu yoyote. Shirika hili lisilo la kiserikali, ambalo linatoa msaada wa kisheria na usaidizi kwa wafungwa wa kisiasa na wapinzani nchini Urusi, sasa limepigwa marufuku, na mtu yeyote ambaye anawasiliana na shirika hili ameonywa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hii si mara ya kwanza kwa shirika hilo lisilo la kiserikali la OVD-Info kulengwa na mamlaka ya Urusi, lakini shambulio hili ni la kikatili zaidi hadi sasa. “Hili ni pigo gumu zaidi. Karibu kazi yetu yote sasa imepigwa marufuku nchini Urusi,” analalamika msemaji wa OVD-Info Dimitrii Anisimov.
Shirika hilo limesitisha ghafla shughuli zake zote nchini Urusi: kuanzia uhusiano wake na mawakili wa wafungwa wa kisiasa hadi usaidizi wote wa kisheria unaotolewa kwa familia zao, miongoni mwa mambo mengine. Kwa kweli, kila mtu ambaye amekuwa na uhusiano wowote na shirika lisilo la kiserikali, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, sasa yuko hatarini. “Nchini Urusi, watu hawawezi tena kutuunga mkono. Hawawezi kutupigia simu ili kuonyesha uungaji mkono wao. Hawawezi kusambaza hati zetu hadharani, au hata kuonyesha nembo yetu hadharani.”
Wananakabiliwa na mashitaka mbele ya mahakama
Lakini kwa Dimitrii Anisimov, shambulio hili la hivi karibuni ni ishara ya utawala ulio katika hatua zake za mwisho, unaowaogopa raia wake: “Hii inatuonyesha kwamba mamlaka ya Urusi hawahisi kama wako katika nafasi thabiti. Uchaguzi wa bunge unatarajiwa msimu huu wa vuli, na mamlaka ya Urusi inalazimika kutoa vitisho ili kuwafanya watu wafikirie kuhusu hatari badala ya kuchukua hatua.”
Dimitrii Anisimov, ambaye yuko uhamishoni nje ya nchi, na timu ya OVD-Info wanaahidi kuendelea na mapambano yao dhidi ya ukandamizaji wa kisiasa nchini Urusi, kwa kutumia njia zingine.