Idadi ya vifo vya muda kutokana na matetemeko mawili ya ardhi yaliyoikumba Venezuela siku ya Jumatano, Juni 24, 2026, inaendelea kuongezeka huku utafutaji wa manusura katika vifusi ukiendelea. Kufikia siku ya Alhamisi jioni, mamlaka ya Venezuela iliripoti vifo vya angalau watu 235. Misaada ya kibinadamu ya kimataifa inaandaliwa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Matetemeko mawili ya ardhi, yenye ukubwa wa 7.2 na kisha 7.5 kwenye kipimo cha Richter, yaliikumba Venezuela siku ya Jumatano, Juni 24, 2026, na kusababisha uharibifu mkubwa, hasa katika mji mkuu, Caracas, ambapo majengo mengi yaliporomoka. Waziri wa Afya wa Venezuela aliripoti idadi ya vifo ya angalau 235 siku ya Alhamisi jioni. Hata hivyo, takwimu hii inaweza kuongezeka sana huku wafanyakazi wa uokoaji wakiendelea na utafutaji wao.

Misaada ya kimataifa inapelekwa. Marekani imetangaza kuwa imetoa dola milioni 150 kama msaada, huku Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akitangaza kutumwa kwa maafisa wauokoaji 85 kwenda Venezuela. iku ya Jumatano, Rais wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodriguez, alitangaza hali ya hatari.

Eneo la La Guaira, kaskazini mwa mji mkuu Caracas, linaonekana kuwa ndilo lililoathiriwa zaidi. Uharibifu uliopo ni mkubwa, na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maiquetia umefungwa. Wakazi wengi wanalaani ukosefu wa msaada kutoka kwa mamlaka na ukosefu wa taarifa rasmi.

Brazil yatangaza vifo vya raia wawili nchini Venezuela

Wabrazil wawili wamefariki kufuatia matetemeko mawili ya ardhi yalilotokea nchini Venezuela, serikali ya Brazil ilitangaza siku ya Alhamisi, na kuongeza kuwa itatuma msaada kwa nchi hiyo jirani.

“Wizara ya Mambo ya Nje inatangaza, kwa masikitiko makubwa, vifo vya raia wawili wa Brazil (mwanamke na mwanaume) kufuatia matetemeko ya ardhi yaliyoikumba Venezuela,” wizara ya Brazil iliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *