Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amelaani “uhalifu mbaya” uliofanywa na Marekani katika shule ya Msingi ya Shajareh Tayyebeh ya Minab nchini Iran wakati wa mashambulizi ya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kislamu, na kutoa wito kwa wahusika wote, wapangaji na viongozi kuwajibishwa kikamilifu, akisisitiza kwamba: “Kumbukumbu ya watoto wa Minab inahitaji haki, uwajibikaji na utekelezaji, si kukaa kimya.”

Amir Saeed Iravani amesema hayo katika mkutano wa kila mwaka wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu “Watoto na Migogoro ya Silaha,” uliofanyika kupitia ripoti ya Katibu Mkuu ya 2025. Amesema: “Ripoti hii haionyeshi vya kutosha athari mbaya kwa binadamu za uchokozi wa siku 12 wa Israel dhidi ya Iran mnamo Juni 2025, haswa athari zake mbaya kwa watoto, kwani watoto 47 wa Iran waliuawa shahidi wakati wa uchokozi huo.”

Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba: “Hatuwezi kujadili ulinzi wa watoto bila kushughulikia mojawapo ya uhalifu mkubwa zaidi wa kivita uliofanywa na Marekani na utawala wa Israel dhidi ya watoto wa Iran.”

Iravani amesisitiza kuwa: “Marekani na jeshi la Israel, kwa makusudi, zililenga raia na miundombinu ya kiraia katika uchokozi wa hivi karibuni dhidi ya Iran. Katika uvamizi huo, shule nyingi na taasisi nyingine za elimu, pamoja na maeneo mengine ya kiraia, yalishambuliwa kwa mabomu na kuharibiwa au kusababisha madhara makubwa. Katika mashambulizi hayo, watoto 220 waliuawa shahidi, wakiwemo watoto 17 waliokuwa na chini ya umri wa miaka mitano.”

Amesema: “Uhalifu mbaya zaidi ulifanyika katika Shule ya Msingi ya Minab katika Mkoa wa Hormozgan (kusini mwa Iran) wanafunzi wakiwa ndani ya shule. Wakati wanafunzi 264 walipokuwa madarasani mwao, shule hiyo ilikumbwa na mashambulizi mawili ya makombora ya Marekani. “

“Uhalifu mbaya zaidi ulifanyika katika Shule ya Msingi ya Minab katika Mkoa wa Hormozgan (kusini mwa Iran) wakati wa masomo. Wakati wanafunzi 264 walipokuwa madarasani mwao, shule hiyo ilikumbwa na mashambulizi mawili ya makombora ya Marekani,” amesema Iravani.

Mashambulizi hayo yaliua shahidi watoto 168, wenye umri kati ya miaka 7 na 12, pamoja na walimu wao na wazazi, na kujeruhi wengine zaidi ya 96. Waathiriwa wengi walinaswa chini ya kifusi kwa saa nyingi, na baadhi ya miili ya wahanga wa mashambulizi hayo iliharibiwa vibaya sana kiasi kwamba haikuweza kutambuliwa.

“Hawa walikuwa watoto wanaotekeleza haki yao ya msingi ya kupata elimu katika eneo ambalo lilipaswa kuwa salama. Walikuwa raia wanaolindwa na sheria ya kimataifa ya kibinadamu,” amesema Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *