
Mwezi Desemba mwaka huu, kwa mara ya kwanza Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Usimamizi wa Matumizi ya Intaneti, IGF utafanyika barani Afrika ukiwa ni mkutano wa 21. Kabla ya hapo, mkutano huo wa Ulimwengu utatakaofanyika Kenya utatanguliwa na mkutano mwingine kama huohuo lakini mahususi kwa bara la Afrika pekee, AfIGF na huo utafanyika mwezi Novemba nchini Ghana.