• Mwigizaji wa Tanzania na aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Wema Sepetu, aliwahi kufunguka kuhusu safari yake ndefu ya changamoto za kupata mtoto
  • Alitangaza kuzaliwa kwa mwanawe mwezi Juni, jambo lililowafanya Watanzania na mashabiki wake duniani kote kumpongeza yeye pamoja na mpenzi wake, Whozu
  • Katika video mpya, alieleza jinsi maisha yake yalivyobadilika tangu ajifungue na kutuma ujumbe kwa watu wanaotilia shaka kuwa ndiye aliyebeba ujauzito

Mwigizaji wa Tanzania Wema Sepetu amewajibu wakosoaji ambao wamekuwa wakizungumza kumhusu tangu alipotangaza kuzaliwa kwa mtoto wake.

Wema Sepetu.
Wema Sepetu amewataka wambea wanaotilia shaka ujauzito wake wamkome. Picha: Wema Sepetu.
Source: Facebook

Mnamo Juni 13, Wema alitangaza kuwa amejifungua mtoto wa kiume, hatua iliyokuwa ya furaha kubwa baada ya safari yake ndefu na ya wazi ya kupambana na changamoto za uzazi.

Kuzaliwa kwa mwanawe kulikuja muda mfupi baada ya mwigizaji huyo kufanya sherehe ya kifahari ya baby shower, ambayo ilikuwa imezua hamasa kubwa miongoni mwa wafuasi wake.

Hapo awali, alikuwa amesimulia jinsi alivyokuwa ameacha kabisa kujaribu kupata mtoto na kumwachia Mungu afanye kila kitu kwa wakati wake.

Pia soma

Picha za kabla na baada ya mwanamke aliyefungwa minyororo na kakake zawaacha wengi wakilia

Hata hivyo, baada ya kujifungua, baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii walidai kuwa alipata mtoto kupitia IVF, huku wengine wakidai hata alitumia mama mbeba ujauzito (surrogate mother).

Wema Sepetu alisema nini kuhusu madai ya IVF?

Hali hiyo ilimfanya Wema pamoja na marafiki zake kushiriki video za zamani (TBT) zikionyesha safari yake ya ujauzito pamoja na video nyingine akiwa hospitalini wakati wa kujifungua.

Katika video iliyoshirikiwa Instagram na @amageneous, Wema pia alizungumza kuhusu jinsi ambavyo bado haamini kwamba sasa ni mama.

“Kuna nyakati namtazama Baby Ollie na kujiuliza, ‘Ina maana wewe ni wangu?’. Hasa anapokuwa ananyonya, namtazama na kusema sikuwahi kufikiria siku kama hii ingefika. Lakini imefika, na ni Mungu pekee. Namshukuru Mungu kila siku. Ninaomba Mungu amlinde dhidi ya kila uovu. Lakini niacheni tu, huo ndio ujumbe wangu pekee. Nimechoka,” alisema.

Tazama video hapa chini:

Baadhi ya maoni kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii

@Naira alisema:

“Sawa tumekubali mtoto ni wako.”

@mwajumashafii207 alisema:

“Huyu si alisema anapumzika kutoka kwenye mitandao ya kijamii?”

@_.itsfermy alisema:

“Wema, nakupenda sana na ninakuombea heri na baraka ziwe juu yako daima Insha’Allah.”

Pia soma

Kanyari apeleka vita vya malezi dhidi ya Tash kortini, adai wanawe wanatumiwa kama silaha

@nabilphdtz alisema:

“Wema usisahau katika furaha zako kumuombea awe mtoto mwema.”

@favorwisdom1 alisema:

“Furaha ya Wema anaijua mwenyewe na Mungu wake. Ukikosa halafu baadaye kwa fadhila na huruma za Mungu ukapata, furaha ndiyo hii. Msimshangae, anaamini ipitayo akili zote.”

@cambodi4568 alisema:

“Dada usijibu kitu ng’o, kimya! Watandike na ukimya wako. Super mama.”

@ephraim_magreth alisema:

“Wapumzike waache kumkausha maziwa mama Ollie.”

Je, Pastor Ezekiel alimwombea Wema apate mtoto?

Katika ripoti nyingine, muda mfupi baada ya Wema kutangaza kuzaliwa kwa mtoto wake, video ya zamani ya Pastor Ezekiel Odero akimwombea ilijitokeza tena mtandaoni.

Video hiyo ilionyesha tukio la zamani ambapo Pastor Ezekiel, baada ya kuguswa na mahojiano ambayo Wema alikiri kwa hisia kuwa alikuwa amekata tamaa ya kuwa mama kutokana na umri wake, alimwombea kwa bidii Mungu ampe muujiza usiotarajiwa.

Katika video hiyo iliyoibuka tena, Wema alionekana akiungana na mhubiri huyo katika maombi kwa kusema “Amina,” jambo ambalo mashabiki walilitaja kuwa unabii wenye nguvu uliotimia baada ya kujifungua salama.

Pia soma

Shiro Stuart Afichua Siri Nzito za Nyumbani kwa Betty Bayo Baada ya Kifo Chake

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Chanzo: TUKO.co.ke

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *