Halmashauri ya Wilaya ya Songea imeweka mikakati ya kutekeleza mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa lengo la kufuta hoja za ukaguzi zilizosalia, kuimarisha uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma, kuongeza mapato ya ndani na kuboresha utoaji wa huduma za maendeleo kwa wananchi.
Hatua hiyo imebainishwa katika Baraza Maalum la Madiwani la kujadili taarifa ya ukaguzi wa mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Ruvuma, Nicholous Killinga, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Songea kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo. Hata hivyo, amesisitiza umuhimu wa kukamilisha utekelezaji wa hoja 20 za ukaguzi pamoja na maagizo mawili ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa ili kuendelea kuimarisha usimamizi wa fedha za umma.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, George Ponela, amesema halmashauri imepokea maelekezo yote yaliyotolewa na tayari imejipanga kuyafanyia kazi kwa wakati, akieleza kuwa lengo ni kuendelea kuboresha utendaji na kudumisha rekodi nzuri ya usimamizi wa fedha za umma.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, amewataka viongozi na watendaji wa halmashauri hiyo kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kusimamia ipasavyo vyanzo vyote vya mapato, kutumia mifumo ya kisasa kwa uwazi na uwajibikaji pamoja na kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuongezeka kwa mapato ya ndani kutaiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Songea kugharamia kwa ufanisi zaidi miradi ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma muhimu kwa wananchi, huku akisisitiza nidhamu ya matumizi ya fedha za umma katika ngazi zote za utendaji.
Baraza hilo pia limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma na kamati yake ya Ulinzi na usalama, Viongozi wa vyaka vya siasa Mkoa, Katibu Tawala wa Wilaya ya Songea, Mtela Mwampamba, pamoja na madiwani na watendaji wa halmashauri, ambapo wote
(Feed generated with FetchRSS)