Matetemeko mawili ya ardhi yaliyoikumba Venezuela siku ya Jumatano, Juni 24, yaligharimu maisha ya watu wasiopungua 920, kulingana na takwimu rasmi za hivi karibuni. Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa anaripoti zaidi ya watu 50,000 hawajulikani walipo. Wakati shughuli ya kuwatafuta manusura nchini ya vifusi likiendelea, hatu za serikali ya Venezuela zinakosolewa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Matetemeko mawili ya ardhi, yenye ukubwa wa 7.2 na kisha 7.5 kwenye kipimo cha Richter, yaliitikisa Venezuela siku ya Jumatano, Juni 24, 2026, na kugharimu maisha ya watu 920 na maelfu kadhaa kujeruhiwa. Lakini idadi hii ya vifo inaweza kuongezeka huku waokoaji wakiendelea na utafutaji wao. Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa aliliambia shirika la habari la AFP kwamba zaidi ya watu 50,000 hawajulikani walipo.

Eneo la La Guaira, kaskazini mwa mji mkuu Caracas, linaonekana kuwa ndilo lililoathiriwa zaidi. Uharibifu ni mkubwa, na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maiquetia umefungwa. Wakazi wengi wanalaani ukosefu wa msaada kutoka kwa mamlaka na uhaba wa taarifa rasmi.

Saa arobaini na nane baada ya matetemeko makubwa zaidi ya ardhi yaliyorekodiwa nchini Venezuela tangu mwaka 1900, timu za utafutaji na uokoaji za kimataifa kutoka angalau nchi 17 zilianza kutoa msaada. Siku ya Ijumaa Marekani ilitangaza kwamba itapeleka timu ya watu 250 katika eneo lililoathiriwa, baada ya kutoa dola milioni 150 na kutuma meli mbili za kivita, ndege za usafiri, na helikopta kusaidia nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *